Sunday 27 July 2014

Ubadilishaji wa Combination kwa Form Five 2014


WANAFUNZI WALIOFAULU SAYANSI



Ni kwa wale waliofaulu vizuri masomo ya sayansi na kupangiwa masomo ya sanaa
Katibu Mkuu Tamisemi Ndugu Jumanne Sagini akiongea na waandishi wa habari katika 
mkutano uliofanyika ofisi ndogo za wizara zilizopo Magogoni Dar es Salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa an Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Ndugu Jumanne Sagini, amesema kuwa wanafunzi wote waliofaulu vizuri masomo ya sayansi na wanapenda kusoma masomo hayo lakini walipangiwa masomo ya sanaa kutokana na kukosa nafasi, wanayo fursa ya kubadilisha kupitia kwa wakuu wao wa shule; na endapo kwenye shule walizopangwa hakuna tahasusi za masomo ya Sayansi wanaweza kuwasilisha maombi yao kwa Maafisa elimu Mikoa ambapo shule hizo zipo, kupitia kwa wakuu wa shule walizopangiwa, ili waweze kubadilishiwa tahasusi za sayansi kwenye shule zilizopo kwenye Mikoa husika.
Ngugu Jumanne Sagini aliyasema hayo katika mkutana na waandishi wa habari uliofanyika tarehe Julai 22, 2014 katika Ofisi za OWM-TAMISEMI, Dar es Salaam.
“Tumetoa maagizo kwa wakuu wa shule na maofisa Elimu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha wanafunzi waliofaulu masomo ya sayansi na kupangiwa sanaa wanabadilishiwa iwapo watataka.” Alisema ndugu Jumanne Sagini.
Aidha ndugu jumanne Sagini alisema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa masomo ya sayansi na mwitikio chanya uliopo sasa kwa wanafunzi kusoma masomo hayo, imeendelea kuimarisha miundombinu ya shule kwa kutoa fedha za ujenzi, ukamilishaji na ukarabati. Pia, Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili kwa wanafunzi waliobaki kutokana na ufinyu wa nafasi za shule za kidato cha tano, baada ya kubaini uwepo wa nafasi hizo; na inatarajiwa kwamba baadhi ya wanafunzi wenye sifa watachaguliwa kwenda kusomea ualimu na vyuo vingine vya ufundi.
Katika matokeo ya mtihani kwa mwaka 2014, inaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 22,685 kati yao Wasichana 7,859 na Wavulana 14,826 wamechaguliwa kusoma tahasusi za sayansi ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 18,746 kati yao Wasichana 5,038 na Wavulana 13,708 kwa mwaka 2013. Aidha tofauti na miaka mingine iliyopita, Ufaulu wa watahiniwa wa shule kwa mwaka 2013 katika madaraja ya I -III umeongezeka kutoka watahiniwa 35,357 mwaka 2012 hadi 71,527 mwaka huu. Ufaulu huu ni zaidi ya asilimia mia moja ya watahiniwa waliokuwa na sifa za kuendelea na masomo ya kidato cha tano mwaka 2013.
“Natoa pongezi nyingi kwa walimu, wanafunzi,wazazi/walezi na wadau wote wa elimu kwa juhudi walizozifanya kuwezesha ufaulu katika masomo ya sayansi kuongezeka kwa kiasi cha kuridhisha.” Alisema ndugu Jumanne Sagini. 
Pia ndugu Jumanne Sagini alieleza kuwa matokeo haliyotangazwa mwaka huu 2014 yanakaribia sana malengo ambayo Serikali imejiwekea kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (yaani Big Results Now-BRN) ambapo serikali ilijiwekea lengo la kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa asilimia 60 mwaka 2013. Matokeo halisi yanaonyesha kuwa ufaulu umepanda kutoka asilimia 43 mwaka 2012 hadi asilimia 58.25 mwaka 2013.
Wakati huohuo shule zote zilizofanya vibaya katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu 2014, ambapo mazingira na nafasi yake iliruhusu kufanya vizuri, zimeamriwa kujieleza sababu za kufanya vibaya.
Ndugu Jumanne Sagini alisema kuwa Makatibu Tawala Mkoa wameagizwa kutoa maelezo na kufanya utafiti ndani ya mwezi kubaini sababu ya shule hizo kufanya vibaya ili hatua stahiki zichukuliwe, hali hiyo isijirudie.
“Tumetaka maelezo kutoka kwa Makatibu Tawala Mkoa; kwa nini shule zimefanya vibaya. Matokeo ya hovyo kama haya ni jambo lisiloweza kueleweka; na wasimamizi wa elimu nimewaambia halikubaliki.” Alsema ndugu Sagini.
Aidha ndugu Sagini aliendelea kusema “Shule kongwe kama Tambaza na Iyunga, zinazopewa fedha na Serikali, zina walimu wa kutosha, zina maabara, nyumba za walimu lakini bado matokeo yanakuwa ya hovyo, tunataka kujua sababu”.
Ndugu Sagini aliendelea kusema: “Sisi wenyewe imetuudhi, imetuhuzunisha na kwa kweli haikuwa matarajio ya Serikali kwa shule kongwe kuwa na matokeo mabaya”.
Hata hivyo alisema kuwa anazo taarifa za kuwepo kwa vikao vya kushughulikia matokeo mabaya katika shule ya sekondari Tambaza iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha aliainisha kuwa tatizo lililochangia baadhi ya shule kufanya vibaya ni kukosa usimamizi makini, hivyo aliwataka wakuu wa shule kutimiza wajibu wao.

















Share:

Saturday 26 July 2014

The Flying Car

Flying Car Company Starts Taking Orders For Its Parajet SkyRunner

flying car
ADVERTISEMENT
If a flying car is something you’ve always wanted and you have enough cash to spare, you could possibly own your own flying car in the near future.
Even though the Parajet SkyRunner isn’t really for sale yet, the company that makes the flying car is ready to start taking orders to bring the prototype to the market, according to Bloomberg. Parajet International Ltd. began enticing customers at the Farnborough airshow in England earlier in the month with it’s $137,000 flying vehicle.
While the car isn’t exactly what you might expect when you think of a futuristic flying machine, the vehicle does operate as a standard off-terrain vehicle and flying machine. It looks more like an all-terrain vehicle that has morphed with a paraglider wing than it looks like a car with hovercraft capabilities.
SkyRunner
This flying car looks like an ATV morphed with a paraglider.
The flying car that anyone can order is a third-generation vehicle, according to Newsmax. Its original predecessor flew and drove successfully from the U.K. to Africa in 2009. Testing in Nevada is currently underway for the most recent model of the flying car.
The SkyRunner flying car has the ability to reach 115 miles per hour on the ground and can fly for up to three hours. Flight time largely depends upon the size of the fuel tank, according to Managing Director Tom Prideaux-Brune.
“We have a lot of interest from the leisure sector, but we’re just evaluating potential uses,” Prideaux-Brune informed the media.
The car may have future military and search and rescue uses.
The flying car has a foot-launched powered paraglider that relies upon the use of a small engine and a propeller that is worn on a backpack upon takeoff. Winds as high as 15 miles per hour can be utilized when using the flying car. The pack weighs about 60 pounds.
According to the product website, “In the unlikely event of engine or wing failure, the SkyRunner simply floats softly to the ground on its paraglider, or a ballistic reserve chute can be deployed.”
Inventor Gilo Cardozo flew the first-generation flying car to Africa and said, “Flying over the desert in a flying car is absolutely surreal. It’s an extraordinary experience. In the right environment, when you’ve learnt to fly, it’s very safe.”
Bear Grylls, the celebrity adventurist, reportedly flew one of these flying cars over Mount Everest, according to Bloomberg.
If you want to fly with your friends in a SkyRunner, you will have to wait. The current flying car can only seat one passenger, but soon you may have luck with other companies working hard to bring flying cars to the main market. Terrafugia, a company out of Massachusetts, already sells it’s fixed-wing plane that doubles as a car. That flying car is called the Transition, and two people can conveniently enjoy the one-of-a-kind ride together.

Share:

Scholarship offer for Form 4


The Tanzania Ministry for Education and Vocation Training has announced it will provide scholarships to Form Four leavers with a Division One ranking in science subjects who will enrol themselves for the diploma in teaching course.
The offer was made public by the Deputy Minister for Education and Vocational Training, Ms Jenista Mhagama, at a public rally here addressed by President Jakaya Kikwete.
She said the ministry will also offer a full loan package for last year’s Form Four leavers with Division Two and Three who specialized in science subjects.
Ms Mhagama, who is also Peramiho MP in the region, said the move is aimed at addressing the shortage of science teachers in public schools. The deputy minister’s announcement comes almost three days after President Kikwete expressed the government’s intention to bring changes in the education sector in which graduates will be teaching in primary schools.
Ms Mhagama said there are 4,000 students currently taking their education degree course at the University of Dodoma (UDOM) and other 30 teacher training colleges countrywide.
She reported that the government has decided to set up a special programme to fill in the gap of science teachers among public schools as part of its objectives to improve the education sector.
“We have managed to address the shortage of teachers in other subjects and the only challenge remaining is for science teachers. But we are on the right track in addressing this too,” Ms Mhagama noted.
She was optimistic that the shortage will end since the government is committed to ending the problem and ensuring that the students are well trained in all fields.
On Sunday, President Kikwete announced massive changes in the education sector, which will see degree holders teaching in primary schools.
He said the programme was expected to take off in a year’s time under which first degree holders would be offered teaching jobs in primary schools to improve the education sector.
The president said the move is aimed at taking education to higher levels, adding that in the developed world; even nursery school teachers have degrees.
He said the country was experiencing positive changes in the performance of ward secondary schools compared to the past
Share:

Kenya's Public University Fees

Public University Fees


 PRESS RELEASE
(Issued under Article 35(3) of the Constitution)
Press Release
 
PUBLIC UNIVERSITY FEES
 
 
 
The Media have carried reports attributed to some stakeholders as expressing concern that the Government intends to increase University fees for students attending public universities.
 
The Ministry of Education, Science and Technology would like to state that it has not sanctioned any university fee increment for any public university. 
 
Reports about planned University fee increment are misleading and inaccurate. Any such increase must be initiated by University Councils, deliberated upon through a consultative process which should involve stakeholders and approved by the Cabinet Secretary for Education, Science and Technology. Key stakeholders in this process include Parliament, Senate, Commission for University Education, Kenya Universities and Colleges Central Placement Service Board, University students’ leadership and parents.  No such process has been started to this effect.
 
 
The Universities Act, 2012 provides for the setting up of the Universities Fund. The Universities Funding Board is the one to determine, in consultation with the public universities, the maximum differentiated unit cost for the academic programmes offered in public Universities.
 
The Ministry wishes to clarify that Vice Chancellors of Public Universities have been working on a model of differentiated Unit cost for financing academic programmes in Public Universities especially through HELB. The Kenya Association of Technical Training Institutions (KATTI) has also initiated a similar exercise to determine the cost of academic programmes under Technical, Vocation Education and Training (TVET) Institutions. The aim is to determine the actual cost of the each degree and diploma programme that Universities and tertiary institutions offer and accordingly peg the cost of each programme on the unit cost.  This process has not been completed.
The Government would like to allay the fears of stakeholders, and particularly University students about the purported increase.
 
In the spirit of inclusive consultations and in order to arrive at a decision on this matter, the Ministry has met the leadership of the National Universities Students’ Organization (NUSO) to inform them about the true position of the matter.  In this respect, all university students are requested not to participate in any disruptive activities especially at this time when many universities are having examinations.
 
 
 
PROF. JACOB T. KAIMENYI, PhD, FICD, EBS
 
 
DATE 19TH MAY, 2014
 
CC:           Chairmen of University Councils
                Vice-Chancellors all Public Universities
                Chairman, Commission for University Education
                NUSO
Share:

Thursday 24 July 2014

Serikali - kuweni macho na matapeli.

                      Serikali - kuweni macho na matapeli.

Na Rose Masaka

Serikali imewataka  wananchi    kujihadhari na wizi ambao hufanywa na Taasisi za Fedha hewa ambazo zimekuwa zikidai kutoa mikopo kwa njia ya simu.Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia  mitandao ya simu za mkononi kutapeli wananchi kwa kuwaraghai kuwa watawapatia mikopo.
Mwambene ameongeza kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia majina ya viongozi wakubwa mbalimbali wa vyama na Serikali kuwatapeli wananchi kwa kuwachukulia fedha zao.Amesema kuwa baadhi ya taasisi hizo zinatumia namba za uongo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwaibia
wananchi.
Mkurugenzi huyo amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni pamoja na Social credit Loans ambayo inadai  imesajiliwa na TRA kwa namba Reg.No.33/SCC/REG/7894 na namba ya utambulisho wa mlipa kodi ni TIN:203-344-6789.
Taasisi nyingine ni Saving Foundation na Quicken Loan ambazo zote hizo zimekuwa zinawatapeli wananchi.Amesema kuwa baada ya kuwasiliana Mamlaka ya Mapato Tanzania, imebainika kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu Taasisi hizo.
Mwambene amesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia uchunguzi ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
Aidha , Mkurugenzi huyo amewakumbusha wananchi kutokubali maombi ya fedha, fadhila au maelekezo yanayodaiwa kutolewa na uongozi wa juu bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika.
Share:

Hadhi ya Tanzania yapanda katika Benki ya Afrika.

                                             THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Tokeo la picha la tanzania logo
          DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS                   
                           
  
   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
Tanzania imepandishwa hadhi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na sasa inaweza kupata mikopo mikubwa zaidi na yenye hadhi kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo katika Tanzania, Bi. Tonia Kandiero ametangaza hayo, Julai 23, 2014.

Bi. Kandiero amesema kuwa miaka yote tokea Tanzania kuwa mwanachama wa AfDB, imekuwa inapata mikopo ya hadhi ya chini zaidi na midogo zaidi ya maendeleo kutokana na uwezo na nguvu za uchumi wake.
Amesema kuwa hadhi ya Tanzania ndani ya Benki hiyo imepanda kutokana na kukua kwa uchumi wa Tanzania, kuongezeka kwa uwezo wa kukopesheka na uwezo wa kulipa na kutimiza masharti yanayokwenda na mabadiliko hayo ya hadhi.Bi. Kandiero ametangaza mabadiliko hayo katika hadhi ya Tanzania ndani ya Benki hiyo wakati alipozungumza katika sherehe kubwa ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya Mangaka-Mtambaswala kwa kiwango cha lami na kufungua Barabara ya Masasi-Mangaka ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami.
Barabara  zote ziko katika mkoa wa Mtwara na mgeni rasmi katika sherehe hiyo kubwa iliyofanyika mjini Mangaka, mji mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ameingia Mkoani Mtwara jana kwa ziara ya siku mbili. Ameingia Mtwara akitokea Ruvuma ambako alifanya ziara ya siku sita.
Bi. Kandiero amemwambia Rais Kikwete na mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo kuwa kabla ya kupandishwa hadhi, Tanzania ilikuwa na sifa za kukopa ndani ya benki hiyo mikopo kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo na siyo mikopo mikubwa ya maendeleo.
Bi. Kandiero amesema kuwa tokea Tanzania kujiunga na AfDB imepata kiasi cha mikopo ya thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni moja. AfDB ni moja ya wafadhili wa barabara hizo mbili ambazo sherehe zake za uzinduzi na jiwe la msingi zimefanyika jana kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania.
AfDB na JICA zinashirikiana na Serikali ya Tanzania kugharimia ujenzi wa barabara hizo chini ya Mradi wa kuendeleza Barabara nchini. Chini ya ushirikiano huo, AfDB inatoa asilimia 64.79 kugarimia ujenzi wa barabara hizo,  JICA inatoa asilimia 31.83 na Serikali ya Tanzania inatoa asilimia 2.39.
Barabaraba ya Mangaka-Mtambaswala, mpakani mwa Tanzania na Mozambique, ina urefu wa kilomita 65.5, inajengwa na kampuni ya Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya shilingi bilioni 59.66 na ujenzi utakuchukua miezi 28.
Nayo Barabara ya Mangaka-Masasi yenye urefu wa kilomita 55.1 ilikamilika mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kuwekewa jiwe la msingi la ujenzi wake na Rais Kikwete Agosti 21, 2009. Barabara hiyo, ilijengwa na kampuni kutoka Japan kwa awamu tatu na kwa gharama ya shilingi  bilioni 54.8.
Barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Masasi-MangakaTunduru.
Mapema jana, Rais  Kikwete amezindua mradi wa maji wa Tarafa ya Nalasi mkoani Ruvuma mjini Nalasi, kilomita 12 kutoka mpakani mwa Tanzania na Mozambique. Mradi huo ambao ni moja ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia utawanufaisha watu 11,655 katika vijiji vitatu.
Mradi huo una uwezo wa kutoa lita 200,000 za maji ambayo yataweza kupatikana katika vituo 37 vya ugawaji maji. Ili kusambaza maji hayo kwa watu wengi zaidi, kiasi cha kilomita 14.5 ya mabomba yametandazwa katika vijiji hivyo.Mradi huo umejengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa gharama ya sh milioni 445.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Julai,2014
Share: