Saturday 30 August 2014

UCHAGUZI WA WANAFUNZI KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2014 - AWAMU YA PILI

      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA TANO 2014 AWAMU YA PILI

Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2014 awamu ya pili.
Wanafunzi 8,101 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili 2014, kati ya hao 4,987 wamepangwa tahasusi za sayansi ya jamii na biashara na wanafunzi 3,114 wamepangwa tahasusi za sayansi.
Wanafunzi hawa wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa kuanzia tarehe 01 Septemba, 2014 na mwisho wa kuripoti ni tarehe 15 Septemba, 2014.

1. Majina ya Wasichana
2. Majina ya Wavulana

Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI
29 AGOSTI, 2014
Share:

Friday 29 August 2014

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUOMBA KAZI SERIKALINI KWA WALIOSOMA NJE YA NCHI, WALIOPOTEZA VYETI NA WENYE MAJINA TOFAUTI NA VYETI VYAO

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUOMBA KAZI SERIKALINI KWA WALIOSOMA NJE YA NCHI, WALIOPOTEZA VYETI NA WENYE MAJINA TOFAUTI NA VYETI VYAO

Sekretarieti ya ajira katika kutekeleza majukumu yake ya uendeshaji wa mchakato wa ajira Serikalini imekuwa ikikabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la baadhi ya waombaji kazi kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa vyeti vya kitaaluma pamoja na vitambulisho vinginevyo. Kutokana na baadhi ya waombaji kazi kutokufahamu taratibu za kufuata pindi wanapopoteza vyeti vyao au wanapobadilisha majina huamua kuwasilisha nyaraka pungufu Sekretarieti ya Ajira jambo ambalo husababisha kukosa nafasi ya kuchaguliwa au kukosa fursa ya kufanya usaili kwa kutokuwa na nyaraka zinazohitajika.

Hali hii imekuwa ikisababisha malalamiko kutoka kwa waombaji kazi wakati wa uhakiki kutokana na baadhi yao kuwa na nyaraka ambazo hazikidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa tangazo la nafasi ya kazi. Kasoro hizo zimechangia baadhi ya wadau kuitupia lawama Sekretarieti ya Ajira kuwa ina upendeleo, kwa kutokuwaita kwenye usaili wale waliobainika mapema kutokuwa na sifa au kuwazuia kufanya usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi na halali ikiwemo vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya taaluma.  Ili kuthibitisha alichowasilisha awali kwa kuwa wengi wao huwa na result slip, hati matokeo (partial transcript) barua  za utambulisho wa upotevu wa vyeti kupitia polisi ambazo baadhi yake huwa zimeshapita muda wake.

Jambo hili limepelekea baadhi ya wahitimu kujikuta njia panda kwa kushindwa kufahamu hatua za kuchukua ama taratibu za kufuata ili kuweza kupata vyeti vingine au namna  ya kufikisha taarifa kwa mamlaka husika ili kuweza kupata msaada ama huduma stahili pindi nyaraka hizo zitakapohitajika mahali fulani. Hivyo, Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu  kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina  kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.

WAHITIMU WALIOPOTEZA VYETI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
Sekretarieti ya Ajira inawataka wadau wake  wote ambao watakuwa wamepotelewa, wameibiwa, wameharibikiwa ama kuunguliwa na Vyeti vya kitaaluma kutambua kuwa wanapaswa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu, pili,  kupeleka taarifa za kupotelewa vyeti katika mamlaka zinazohusika kama vile Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa vyeti vya kidato cha nne(4) na sita(6), kwa Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na kwa elimu ya juu ni Tume ya Vyuo Vikuu(TCU) ili waweze kuelekezwa taratibu za kufuata ikiwemo kutoa tangazo katika vyombo vya habari na maelekezo mengine yatakayomwezesha  kupata vyeti vingine ama taarifa za upotevu wa vyeti kutumwa Sekretarieti ya Ajira kwa wakati.

WAOMBAJI WALIOSOMA NJE YA NCHI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
Sekretarieti ya Ajira pia inawasisitiza  waombaji kazi wote waliosoma Nje ya Nchi iwe ni elimu ngazi ya Sekondari au Vyuo Vikuu kwamba mara tu baada ya kumaliza mafunzo wahakikishe wanapeleka taarifa zao hasa Vyeti vya taaluma kwenye mamlaka husika mapema ili kuhakikiwa taarifa zao na kupewa barua zinazothibitisha kutambuliwa kwa Vyuo walivyosoma ambapo mamlaka zenye dhamana ya kuhakiki taarifa hizo ni Tume ya Usimamizi wa Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE). Kwa kuwa mamlaka hizo ndio zenye dhamana kuthibitisha ama kuwasilisha taarifa za mhusika za kupotelewa na vyeti katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa Mchakato wa Ajira Serikalini na sio mtu aliyepotelewa kuwasilisha utambulisho wa matokeo ama nyaraka mbalimbali zikiwemo za kitaaluma wakati anapoomba kazi.

WAOMBAJI WENYE MAJINA TOFAUTI KWENYE VYETI WAZINGATIE YAFUATAYO;-
Kutokana na baadhi ya wadau wetu kubadilisha majina yao kwa kutokupenda kuendelea kutumia majina ya utotoni, ya kinyumbani au kubadili dini, kuolewa na kutumia ubini wa mume au kurithi majina ya walezi hali ambayo imechangia wengi wao kuwa na majina tofauti kati ya cheti kimoja na kingine iwe cha kuzaliwa ama cha kitaaluma, Sekretarieti ya Ajira inawataka wale wote wenye tofauti ya majina katika vyeti vyao kufuata taratibu za kisheria kabla ya kuwasilisha maombi ya kazi Sekretarieti ya Ajira kwa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa Wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity)  kwa mujibu wa sheria, na sio kubadili majina kienyeji hali ambayo inaweza kuwanyima haki zao wakati mwingine. Kwa kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina au majina yake yote kutambulika kisheria.

Mwisho waombaji kazi wote wenye matatizo ya Vyeti wanashauriwa kuzingatia na kufuata utaratibu ulioelekezwa  mara tu baada ya kupata matatizo ili taarifa zao ziweze kufika mapema Sekretarieti ya Ajira na pia inaweza kuzuia uwezekano wa aliyeiba au kuviokota kuvitumia. Aidha, itawasaidia wakati wanapoomba kazi kuepuka usumbufu na gharama zisizokuwa na ulazima.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Barua pepe: katibu@ajira.go.tzgcu@ajira.go.tz,
Tovuti; www.ajira.go.tz, S.L.P. 63100 Dar es Salaam.
Simu; 255-687624975
Share:

Thursday 28 August 2014

MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA MICHEPUO NA TAHASUSI ZA KIDATO CHA KWANZA HADI KIDATO SITA


Elimu ya sekondari katika ngazi ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne   imekuwa ikiongozwa na michepuo ya ama ya Sanaa, Sayansi, Ufundi na Biashara. Halika dhalika, masomo ya sekondari Kidato cha Tano na Sita yamekuwa ya kifundishwa kwa kutumia Tahasusi mbalimbali kulinga na mahitaji ya nchi ambazo kwa sasa ni PCM, PCB, PGM, CBG,EGM,CBA,CBG,CBN kwa Sayansi, na  HGL, HGK, HKL, KLF, ECA, HGE kwa Sanaa.

Mafanikio mbalimbali yamepatikana kwa kutumia mfumo huu tangu ulipoanza hadi sasa. Hata hivyo, kutokana na (a) nia ya nchi kupiga hatua zaidi katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya nchi kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, (b) mabadiliko ya mahitaji ya ulimwengu wa ajira na kazi na (c) kuendelea kukua kwa ugunduzi na ubunifu pamoja na matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika maeneo mbalimbali, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeona kuna umuhimu wa kupitia upya Michepuo na Tahasusi zilizopo ili ufundishaji uweze kwenda na wakati. Michepuo na Tahasusi hizo mpya zinatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka wa masomo 2015/2016.

Ili kufanikisha maboresho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inakaribisha wadau wote wa Elimu na Mafunzo kutoa mapendekezo ya jinsi gani Michepuo na Tahasusi za elimu ya sekondari ziundwe au kuanzishwa katika madarasa ya kidato cha Kwanza hadi Nne na Tano hadi Sita. Mwisho wa kutuma mapendekezo ni tarehe 31/10/2014. Wadau wote mnahamasishwa kutoa maoni yenu kupitia njia mbalimbali ikiwemo vikao ama kwa kuwasiliana moja kwa moja na wizara. Majumuisho ya mapendekezo ya tawekwa kwenye magazeti na tovuti kwa maoni na hatua za mwisho katika kukamilisha maboresho haya.

Mapendekezo ya Michepuo naTahasusi mpya yatumwe kwa anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
7 Mtaa wa Magogoni,
11479 DAR ES SALAAM.

"Elimu Bora Inawezekana; Timiza Wajibu Wako"

KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Share:

CHEVENING SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE UNITED KINGDOM FOR THE YEAR 2014

The Ministry of Education and Vocational Training is inviting applications from qualified Tanzanians for a one- year Masters Degree under the Chevening Scholaships Program tenable in the United Kingdom in the year 2014/2015.

The Chevening Scholarships will cover:
· Tuition fees;
· A living allowance at set rate (for one individual);
· An economy class return airfare to the UK; and
· An additional allowance package.

Qualifications 
· Applicants must be holders of bachelor degree with upper second class honours degree
· Applicants must be completed at least two years work or equivalent experience before applying for a Chevening Scholarship
· Applicants must be able to meet the Chevening minimum English language requirement
· Applicants must be able to obtain the correct visa, and receive an unconditional offer from a UK university.
· Further details of the eligibility criteria can be found at www.chevening.org/apply/ guidance

Mode of Application:
· All applications should be made online to the Chevening Scholarship through the Chevening Scholarships website before the closing date
·It is important that applicants before applying online, should read and understand all given instructions, and should attach all necessary attachment such as certified photocopies of academic certificates, transcripts, birth certificates and submit online through the below indicated link.
· Applicants must specify three courses according to your precedence that you wish to study to three universities and submit to these universities at the same time as, or before applying for a chevening Scholarships
· Applicants must demonstrate how you meet the chevening Scholarships selection criteria in your application.
· Further details of the online application process can be found at www.chevening.org/apply

All applicants who wish to be nominated by the Ministry of Education and Vocational Training, should print one hard copy of completely filled application form, attach with certified photocopies of academic certificates, transcripts, and birth certificate and submit them to the address below before 15th October, 2014.

The Permanent Secretary,

Ministry of Education and Vocational Training,

7 Magogoni Street,

P. O. Box 9121,

11479 DAR ES SALAAM.

icon CHEVENING SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE UNITED KINGDOM FOR THE YEAR 2014-2015 (56.92 kB)
Share:

Wednesday 27 August 2014

ANNOUNCEMENT FOR NOMINATION OF CANDIDATES FOR MEDIATION TEAM



ANNOUNCEMENT FOR NOMINATION OF CANDIDATES FOR THE DEPARTMENT OF POLITICAL AFFAIRS’ STANDBY TEAM OF MEDIATION AT THE UNITED NATIONS SECRETARIAT.
      
 We wish to inform the general public that the United Nations Secretariat, through the Department of Political Affairs (DPA) is seeking the nomination of candidates for the 2015 Standby Team of Mediation Experts to undertake mediation assignments effective from February 2015, for a one-year term. 

         The Team once duly constituted will be composed of eight experts whose work shall concentrate on the following thematic areas: (1) constitutional-making; (2) natural resources; (3) power-sharing arrangements; (4) gender and inclusion issues; (5) security arrangements; and (6) mediation and dialogue process design (three positions).   

         Please note that member of the Team are engaged on a full-time basis with the DPA, and deploy on short notice to the field in support of ongoing good offices and mediation work. In between deployments, the experts carry out research and analysis on mediation issues, as defined by DPA. 


          The deadline for submission of nomination (including the full name, title, contact details and resumes of the nominees) is 14 September 2014. Nomination of women with knowledge of French and Arabic languages is highly encouraged. Supplementary information about the Standby Team of Mediation may be retrieved from the following site: http://peacemaker.un.org/mediation-support/stand-by-team.  
Share:

UHAMISHO WA WALIMU WA VIBALI MAALUMU -, JULAI & AGOSTI 2014

   

Agosti 26, 2014: UHAMISHO WA VIBALI MAALUMU - WALIMU, JULAI & AGOSTI 2014
Tangazo la Uhamisho        
Orodha ya Watumishi        
           

Julai 11, 2014: UHAMISHO WA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA MWEZI JUNI 2014
Tangazo la Uhamisho wa Watumishi        
Orodha ya Watumishi wa Serikali za Mitaa Waliokubaliwa Kuhama        
Orodha ya Watumishi wa Serikali za Mitaa Ambao Hawajakidhi Vigezo vya Kuhama
           

Juni 30, 2014: WALIMU WAPYA
Tangazo la Ajira        
Walimu wa Astashahada        
Walimu wa Stashahada        
Walimu wa Shahada        

Juni 23, 2014: AJIRA KWA WALIMU WAPYA NA VITUO WALIVYOPANGIWA
Tangazo la Ajira        
Walimu wa Astashahada        
Walimu wa Stashahada        
Walimu wa Shahada        

Mei 14, 2014: WATUMISHI WALIOHAMA KWA VIBALI MAALUMU
Orodha ya Watumishi Waliohama kwa Vibali Maalumu        

07/04/2014: WALIMU WA AJIRA MPYA 2014 WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO -                                                   AWAMU YA TATU NA YA MWISHO
Tangazo        
Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi        
Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule za Sekondari        
Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari        

03/04/2014: MAREKEBISHO MAPYA - WALIMU WA AJIRA MPYA 2014 WALIOKUBALIWA                                     KUBADILISHIWA VITUO, WALIOREKEBISHIWA MIKOA NA ORODHA YA NYONGEZA                                                          TOKA SJUT DODOMA
Tangazo        
Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi        
Marekebisho Orodha ya Walimu Waliorekebishiwa Mikoa - Cheti        
Walimu Wapya Toka Chuo Cha SJUT        
Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule za Sekondari        
Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari        

30/03/2014: WALIMU WA AJIRA MPYA 2014 WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO
Tangazo        
Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi        
Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari        
Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari        
           

15/03/2014: AJIRA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI                                                                                        NA SEKONDARI NA VYUO MWAKA 2013/14
Tangazo        
Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi 17,928        
Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari 5,416        
Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari 12,677        
Wallimu Wa Shahada Waliopangwa Vyuoni      

UHAMISHO WA WATUMISHI DESEMBA 2013
Watumishi waliokidhi vigezo vya kupata vibali vya uhamisho        
Watumishi waliohama kwa vibali maalumu        
Watumishi ambao hawakukidhi vigezo        
   
Share: