Wednesday 29 April 2015

Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015.


Image result for tanzania emblem
 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER'S OFFICE
REGIONAL ADMINISTRATION & LOCAL GOVERNMENT - PMORALG
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa.

kwa Maelekezo zaidi tafadhali soma taarifa zifuatazo:











Share:

EAST AFRICAN ESSAY WRITING COMPETITION 2015

Image result for east africa community
The East African Community Secretariat has organized the EAC students essay writing competition year 2015. The Essay writing competition is intended to broaden knowledge of the school going population on EAC activities. The topic for year 2015 in English is “Why is political stability important for the intergration of East African Community Partner States” In Kiswahili is “Jadili umuhimu wa utulivu wa kisiasa katika mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki” The competition is open to students in Form 1 to form 4 who are required to write essays between 1000 – 1500 words. The students are required to begin researching on the topic prior writing and submitting to their Heads of Schools by 15th June, 2015. The Heads of Schools will then be expected to constitute a marking panel which will choose best essay of the school. The panel should go through the essays (Please do not mark the essays) and choose three essays to be submitted to Permanent Secretary Ministry of Education and Vocational Training by July 30th 2015.
  • The following are the guidelines for essay competition
  • The length of the essay should be between 1,000 and 1,500 words,
  • The essay can be written in English, French or Kiswahili,
  • The essay should be in their own hand writing
  • Students information such as name, sex, class, school address, region Country and title of the essay should be written in the cover page,
  • The essay should be written on white A4 lined/ruled papers (Similar to the draft pads),
  • Written only on one side of the paper,
  • The Head of Schools to certify that the essay is student’s own work.
Thank you for your cooperation.
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING
Share:

Saturday 25 April 2015

Majukumu Ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri,Madiwani,Viongozi wa Vijiji,Mitaa na Vitongoji.

Image result for TANZANIA EMBLEM

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
 
1.0 UTANGULIZI
Kwa mujibu wa ibara ya 145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa ni vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma katika sehemu zao. Serikali za Mitaa huanzishwa kwa madhumuni ya kuwahudumia wananchi na kuwapelekea madaraka kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Sifa muhimu zinazozitambulisha Serikali za Mitaa ni pamoja na:
  1. Kuundwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria.
  2. Ni vyombo vya wananchi ambavyo huundwa, huendeshwa, husimamiwa na kuwajibika kwa wananchi.
  3. Hujenga demokrasia kuanzia ngazi ya msingi.
  4. Huleta maendeleo ya wananchi kwani ziko karibu nao.
  5. Ni vyombo vya uwakilishi wa wananchi katika Serikali
Tafadhali bofya hapa chini Kwa Ufaanuzi wa kina.
Share:

Taarifa kwa Umma kuhusu Recruitment Portal

Image result for tanzania emblem
Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma hivi karibuni ilianzisha majaribio ya kupokea maombi kazi kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia ‘Recruitment Portal’ ikiwa ni hatua za majaribio kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mfumo huu hivi karibuni.
Tangu kuanza kwa majaribio ya mfumo huo hivi karibuni, matangazo ya kazi matano (5) yametangazwa na kuwalekeza waombaji kazi kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo huo wenye anuani http://portal.ajira.go.tz  ambapo tathmini inaonyesha kuwa na mafanikio.
Matangazo ya nafasi za kazi ambayo tayari Sekretarieti ya ajira imeyatangaza kupitia mfumo huo yalitangazwa kwa niaba ya Wakala wa Serikali Mtandao(e-GA) la tarehe 22 Aprili, 2014, Tangazo la Mkemia kuu wa Serikali la tarehe 4 Desemba, 2014 na Tangazo la mamlaka ya hali ya hewa(TMA) la tarehe 4 Desemba, 2014 ambayo tayari mchakato wake wa ajira umeshakamilika.
Aidha matangazo ya kazi yaliyobaki ambayo ni tangazo la nafasi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi la tarehe 16 Januari, 2015 taratibu za kuwaita waliofaulu kwa ajili ya usaili zinaendelea. Matangazo mengine mawili yalitangazwa tarehe 10 Machi, 2015 na mchakato wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya ‘Recruitment portal’ unaendelea hadi tarehe 25 Machi, 2015.

Sekretarieti ya ajira imelazimika kutoa ufafanuzi kwa umma kupitia taarifa hii ili kukanusha baadhi ya taarifa zinazosambazwa kuwa utaratibu wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya posta umefungwa rasmi.

Ukweli ni kwamba mchakato wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya posta bado unaendelea na hata sasa baadhi ya matangazo yaliyotangazwa kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz yanahitaji waombaji kutuma maombi yao kupitia posta isipokuwa kwa matangazo tajwa mawili ya tarehe 10 Machi, 2015 ambayo waombaji wameelekezwa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao. Hivyo tunawahimiza waombaji kazi kusoma matangazo hayo kwa umakini kabla ya kutuma maombi yao ya kazi.

Katibu wa Sekretarieti ya ajira anapenda kuwasisitiza wananchi hususani waombaji kazi kuwa ofisi yake inaendelea na uimarishaji wa mfumo mpya wa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao (recruitmemnt portal) ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika na anawasisitiza waombaji kazi waendelee kujisajili katika mfumo huo mpya kwa kuingiza taarifa zao mbalimbali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 17 Machi, 2015.

Attachments:
Download this file (Recruitment Portal User Manual.pdf)How to apply[How to apply]2285 Kb
Share:

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI : Mfumo mpya wa upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao kuzinduliwa hivi karibuni.

Image result for tanzania emblem
Mfumo Mpya wa Upokeaji wa Maombi ya Kazi kwa Njia ya Mtandao Kuzinduliwa Hivi Karibuni.

Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma inatarajia kuzindua mfumo mpya wa utumaji na upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao kupitia “Recruitment portal” hivi karibuni baada ya hatua za majaribio ya mfumo huo kuonyesha mafanikio.
Sababu za kuanzisha mfumo huu mpya zinalenga kuboresha utendaji kazi wa taasisi katika kufikisha huduma kwa wateja, kuongeza ufanisi katika mchakato wa ajira, Kupunguza muda wa mchakato wa Ajira ili kukidhi mahitaji ya wadau, kuwafikia waombaji wa nafasi za kazi wengi zaidi, kudhibiti udanganyifu wa sifa toka kwa waombaji wa fursa za Ajira kwa kurahisisha ukaguzi na uhakiki wa taarifa za waombaji  kazi kwa kuunganishwa na mifumo ya taasisi mbalimbali lakini pia kukidhi maelekezo ya Sera mbalimbali za utumishi wa umma pamoja na dira ya Taifa ya mwaka 2025 kuhusiana na umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kutimiza malengo ya Taifa.
Hadi sasa Sekretarieti ya ajira imefanya majaribio ya kupokea maombi ya kazi kwa kutumia mfumo wa “Recruitment Portal” kwa matangazo ya kazi matano ambayo yaliyowahusu waajiri mbalimbali serikalini na muitikio umeonekana kuwa mzuri.
Matangazo hayo yalihusu Wakala wa serikali mtandao lililotolewa tarehe 22 Aprili, 2014 ambapo kati ya nafasi 12 zilizotangazwa idadi ya maombi yaliyopokelewa yalikuwa 1,158, Tangazo la nafasi za Mkemia mkuu wa Serikali lililotolewa tarehe 4 Desemba, 2014 lenye nafasi 11 jumla ya maombi ya kazi 119 yalipokelewa kwa njia ya mtandao.
Matangazo mengine ni ya  Mamlaka ya Hali ya hewa la tarehe 4 Desemba, 2014 lililokuwa na nafasi  moja na idadi ya maombi ya kazi matatu yaliyopokelewa, tangazo la tarehe 16 Januari, 2015 la Wizara ya Ardhi lililokuwa na nafasi 51 ambalo jumla ya maombi ya kazi 738 yaliwasilishwa na tangazo la mwisho lilitolewa tarehe 10 Machi, 2015 kwa niaba ya taasisi mbalimbali Serikalini jumla ya maombi ya kazi 2,567 yalipokelewa kutumia mfumo huu. Idadi hii inaonyesha kuwa watu wengi wameanza kuhamasika na matumizi ya mfumo huu.
Taratibu za uzinduzi rasmi wa mfumo huu inatarajiwa kufanyika hivi karibuni ambapo sekretarieti ya ajira inatarajia kupunguza muda wa uendeshaji wa  mchakato wa ajira kwa asilimia 34%. Aidha mfumo pia utapunguza changamoto kadhaa zikiwemo baadhi ya barua kutofika kwa wakati au kupotea kwa kutumia njia ya posta, Mrundikano wa barua na nyaraka nyingine zinazohusiana na maombi ya kazi  kutokana na matumizi ya karatasi, Barua za vibali vya ajira kuwasilishwa wakati vimechelewa na kusababisha mchakato kuchelewa na gharama inayotokana na uendeshaji wa mchakato mzima wa ajira kuwa juu.
Pia mfumo huu utakuwa rafiki na rahisi kwa watumiaji kwa kuwa wataweza kutumia simu zao za kiganjani kupata taarifa za mchakato wa ajira kila wakati kwa kupiga *152*00#
Tunatoa rai na kusisitiza kuwa waombaji kazi na wale wanaotarajia kuingia katika soko la ajira wajisajili katika mfumo huu kwa kufungua http://portal.ajira.go.tz ili kuingiza taarifa zao za kitaaluma, wasifu binafsi (CV) pamoja na vyeti.
Matarajio ya Sekretarieti ya ajira ni kuona kuwa mara baada ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi utaongeza ufanisi, ubora, uwazi na uwajibikaji wa huduma zinazotolewa, kupunguza muda unaotumika sasa wa kuendesha mchakato wa ajira, Gharama za uendeshaji zitapungua kwa kiasi kikubwa na mfumo utawafikia waombaji wa fursa za kazi wengi zaidi na kwa haraka.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitiza wananchi hususani waombaji kazi kuwa inaendelea na uimarishaji wa mfumo mpya wa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao (recruitmemnt portal) ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizojitokeza baada ya majaribio kabla ya uzinduzi wake na tunasisitiza na kuhimiza waombaji kazi pamoja na wanafunzi wanaotarajia kumaliza vyuo waendelee kujisajili katika mfumo huo mpya.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma
Share: