Tunapenda kufafanua kuwa taarifa zinazosambazwa katika baadhi ya
mitandao ya kijamii kuwa orodha ya majina ya waombaji wa Mikopo
waliofanikiwa kwa mwaka wa masomo 2015/2016 imetoka sio za kweli. Kwa
sasa, kazi ya uchambuzi wa maombi ya mikopo yaliyowasilishwa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu bado inaendelea.
Mwisho.