Sunday 11 December 2016

JKT: TANGAZO KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016


TAARIFA KWA UMMA

1.    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawatangazia vijana wa Kitanzania wito wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na Vijana wa Kujitolea.

2.    Vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:-

      a.   Vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.
             Kundi hili linahusisha wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu  wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga vyuo vya elimu ya juu. Aidha, orodha kamili ya majina na makambi waliyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambayo ni www.jkt.go.tz  na Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz

      b.      Vijana wa Kujitolea
Kundi hili linahusisha Vijana wote waliosailiwa mwezi Mei na  Juni mwaka 2016 katika ngazi za wilaya na mkoa  na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.
3.   Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:
      a.  Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza (Dark blue) yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma isiyo na zipu, iwe na urefu  unaoishia magotini.                 

       b.  Raba ngumu za michezo zenye rangi ya kijani au nyeusi.

       c.  Shuka jozi mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari ukubwa wa 4x6.
       d.  Soksi za michezo jozi mbili rangi nyeusi.

       e.  Chandarua moja ya duara rangi ya bluu au kijani ukubwa wa 4x6.

        f.  Nguo za michezo (truck suit) jozi moja rangi ya kijani au bluu.

        g.  Fulana (T-shirt) ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote.

        h.  Mavazi hayo yasiwe ya kubana mwili.

4.  Inasisitizwa kuwa vijana wa kujitolea wanaotakiwa kuripoti makambini ni wale tu waliopita katika usaili kwenye ngazi
za wilaya na mikoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.

5.  Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na  Kujitolea wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia
tarehe 01 mpaka 05 Desemba 2016 kwa kujitegemea nauli ya kwenda na kurudi.

 BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI  2016  

BULOMBORA JKT-KIGOMA                     

      RWAMKOMA JKT -MARA         
         MSANGE JKT-TABORA

KANEMBWA JKT-KIGOMA                
                         MTABILA-KIGOMA            
          RUVU JKT-PWANI

MAKUTUPORA JKT- DODOMA                  
         MGAMBO JKT-TANGA        

MAFINGA JKT- IRINGA                                
                                       MLALE JKT -RUVUMA


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 17 Novemba 2016
Share:

JKT: KUONGEZWA MUDA WA KUPOKELEWA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016




TAARIFA KWA UMMA

Jeshi   la   Kujenga   Taifa   kwa   mara   nyingine   tena, 
linawatangazia wanafunzi wote waliohitimu kidato cha
sita   mwezi   Mei   2016,   ambao   hawakuchaguliwa
kujiunga   na   mafunzo   ya   JKT   Mujibu   wa   Sheria
Operesheni   Magufuli   Awamu   ya   Kwanza   na
hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya
juu, kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa
kabla ya tarehe 13 Desemba 2016 .
Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linaukumbusha umma
kuwa   ni   kosa   la   jinai   kwa   kijana   aliyetangaziwa
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria
kushindwa kujiunga na mafunzo hayo.
Kosa hilo la jinai, ni kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la
Kujenga Taifa, Sura Namba 193 ya mwaka 1964 na
kufanyiwa mapitio mwaka 2002 kifungu cha 11 kifungu
kidogo cha (8).
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mwanafunzi
yeyote   atakayeshindwa   kuripoti   ndani   ya   muda
uliopangwa   wa   kuanza   mafunzo   ya   JKT   Mujibu   wa
Sheria   Operesheni   Magufuli   Awamu   ya   Pili   mwaka
2016.


Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 07 Desemba 2016

Share:

HESLB: WADAIWA SUGU KUHUDUMIWA IJUMAA, JUMAMOSI NA JUMAPILI

Image result for WANAPORTAL HESLB

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya zoezi la kuwataka wadaiwa sugu kulipa madeni yao ndani ya siku 30, Ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitakuwa wazi kwa siku tatu, Ijumaa, Disemba 09, 2016,  Jumamosi, Disemba 10, 2016 na Jumapili, Disemba 11, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao kupata taarifa kuhusu madeni yao na kulipa.
Njoo na Majina yako kamili, Chuo ulichosoma, Mwaka wa kuanza na wa kuhitimu, anuani yako ya barua pepe (email), nambari ya simu yako ya kiganjani, mwajiri wako na Check Number yako iwapo umeajiriwa serikalini.
Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu kabla ya zoezi kuhitimishwa na hatua za kisheria kuanza kuchukuliwa.
‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’
Kwa mawasiliano zaidi piga 0763 459165 au 0767 513208
 

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
08/12/2016
Share:

HESLB: Orodha ya WADAIWA SUGU

Image result for WANAPORTAL HESLB
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995. Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi. 

Kwa mawasiliano zaidi piga 0763 459 165 au 0767 513 208 au tembelea ofisi zetu za Makao Makuu, Dar es salaam au ofisi zetu za kanda zilizopo Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha.

INSTITUTIONS LIST

S.NoInstitution NameCode
1Zanzibar UniversityZU
2Zanzibar Institute of Finance & AdministrationZIFA
3Water Development & Management Institute(Chuo cha Maji - Ubungo)WDMI
4University of DodomaUDOM
5University Of Dar Es SalaamUDSM
6University of ArushaUOA
7Tumaini University Makumira CampusMUCO
8Tumaini University KCMC CampusTUKCMC
9Tumaini University Iringa CampusTUICO
10Tumaini University Dar es salaam CampusTUDARCO
11Teofilo Kisanji UniversityTEKU
12Tanzania Institute of AccountancyTIA
13Stephano Mosha Memorial University CollegeSMMUCO
14State University of ZanzibarSUZA
15St.John's University of Tanzania DSMSJUTDSM
16St.John's University of TanzaniaSJUT
17St. Joseph University in Tanzania, Arusha CampusSJUTAC
18St. Joseph College of EngineeringSTJCE
19St. Augustine UniversitySAUT
20Sokoine University of AgricultureSUA
21Sebastian Kolowa University CollegeSEKUCO
22SAUT MtwaraSAUTMTR
23Ruaha University collegeRUCO
24Primary Healthy Care InstitutePHCI
25Overseas InstitutionsOVERSEAS
26Open University of TanzaniaOUT
27Not ApplicableNTAPP
28Newman Institute of Social WorkNISW
29National Institute of Transport.NIT
30Mzumbe UniversityMU
31Mwenge University College of EducationMWUCE
32Mwalimu Julius K. Nyerere University of Agriculture and TechnologyMJNUAT
33Mwalim Nyerere Memorial AcademyMNMA
34Muslim University of MorogoroMUM
35Muhimbili University of Health and Allied SciencesMUHAS
36Mount Meru UniversityMMU
37Moshi University College of Cooperatives and Business Studies.MUCCOBS
38MODERN COMMERCIAL INSTITUTEMCISTU
39Mlimani School of Professional Studies - Dar es SalaamMLIMANI
40Mkwawa University College of EducationMUCE
41Mbeya Institute of TechnologyMIST
42Masoka Management Training InstituteMASOKA
43KAM College of Health Sciences -DSMKAM
44JORDAN UNIVERSITY COLLEGE-MOROGOROJUCM
45International Medical and Technological UniversityIMTU
46Institute of Social WorkISW
47Institute of Rural Development PlanningIRDP
48Institute of Jounalism & Mass CommunicationIJMC
49Institute of Finance ManagementIFM
50Institute of Adult EducationIAE
51Institute of Accountancy ArushaIAA
52ILEMI POLYTECHNIC COLLEGE-MBEYAIPCM
53Hubert Kairuki Memorial UniversityHKMU
54Eckensford Tanga UniversityETU
55Eastern and Southern African Management InstituteESAMI
56DSM Maritime InstituteDMI
57Dar es salaam University College of EducationDUCE
58Dar es salaam Institute of TechnologyDIT
59Community Development Training InstituteCDTI
60College of Engineering & TechnologyCOET
61College of Education ZanzibarCEZ
62College of Business Education(DSM campus)CBE
63College of Business Education(Dodoma campus)CBE DODOMA
64College of African Wildlife Management MwekaMWEKA
65Bugando College of Health SciencesBUCHS
66Arusha Technical CollegeATC
67Ardhi UniversityARU
68Agakhan UniversityAKA
Share: