Wednesday 27 August 2014

Rais, wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe, Dkt. Ali Mohamed Shein awaapisha viongozi mbalimbali

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

Zanzibar 25.8.2014

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali
Mohamed Shein jana amewaapisha viongozi mbali mbali wakiwemo Mhe.
Dk. Sira Ubwa Mamboya, kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili. Mhe. Juma
Duni Haji kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Mhe.
Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Afya. B
Wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa
Naibu Waziri wa Afya, Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Mhe Omar Khamis Othman Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba, Mhe. Mwanajuma Majid Abdulla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,
Mhe. Ayub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi pamoja na
Mhe.Hanuna Masoud Ibrahim kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali
akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Mkuu wa Mkoa
wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Meya wa Manispaa
ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na
viongozi wengine wa Serikali.
Kabla ya Uteuzi huo, Dk. Sira Ubwa Mamboya alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya ambaye hivi sasa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa
Wizara hiyo, Mhe. Suleiman Othman Nyanga. Mhe. Juma Duni Haji alikuwa Waziri
wa Afya ambaye hivi sasa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Rashid Seif Suleiman
Ambapo, Mhe. Rashid Seif Suleiman alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
ambaye hivi sasa najaza nafasi iliyowacha wazi na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juma
Duni Haji.
Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba ambaye
kwa hivi sasa anajaza nafasi iliyowachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo
Mhe. Pembe Juma Khamis, Mhe.Mwajuma Majid Abdulla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya
ChakeChake Pemba ambaye kwa hivi sasa anajaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa huo Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa.
Mhe. Omar Khamis Othman alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete ambaye hivi sasa
najaza nafasi iliyowachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Dadi Faki
Dadi, Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud alikuwa Afisa Tawala Mkoa wa Mjini
Magharibi ambaye hivi sasa anajaza nafasi iliyowachwa na aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya hiyo, Mhe. Hassan Mussa Takrima.
Mhe.Hanuna Masoud Ibrahim alikuwa Afisa Tawala Mkoa wa Kusini Pemba ambaye
hivi sasa anajaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Mwanajuma Majid
Abdulla.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza jana tarehe 24 Agosti 2014.
Share:

0 comments:

Post a Comment