Thursday 21 August 2014

Ujumbe wa Wiki ya Uadilifu


UJUMBE WA WIKI WA UADILIFU KUANZIA TAREHE 21 AGOSTI, 2014 HADI 28 AGOSTI, 2014

“UBORA WA KAZI”

Miongoni mwa watu mashuhuri katika uadilishaji umma ni Hayati Shaaban Robert mtazamo wake katika kazi (Mwanafalsafa wa fasihi).

i.   Dharau ya Kazi
ii.   Kazi ni Faradhi (lazima)
iii.   Majivuno ya heshima ya uongo
iv.   Watu bora hawatahayari (hawaogopi) kazi
v.   Watu walioelimika na ubora wa kazi
vi.   Huakikisha maendeleo ya watu na taifa

Dini zote zimehubiri mapenzi ya kazi. Agano la kale (Mwanzo 3:19) inaeleza “kwa jasho la uso wako utakula chakula chako". “Katika Uislamu inaelezwa kuwa, “uvivu ni dhambi”.
Chakula kipatikanacho bila kazi ni sawa na chakula kipatikanacho kwa wizi” ameangalia kazi katika dunia ya leo, “kwa maendeleo ya ustaarabu tumeanza kudharau kazi, ustaarabu wetu wa sasa umetupa nafasi kubwa lakini umetufundisha kuchukia kazi. Ametoa onyo kwetu kwa kutuadilisha”

“NI UJINGA KUDHARAU KAZI” (Shaaban Robert, ukurasa wa 38 - kielelezo cha insha 1954)
Kazi ni faradhi katika maisha. Dhana hii imehitimishwa na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma (ukurasa 10) umezungumzia “BIDII YA KAZI” Tukifanya kazi kwa bidii, Taifa letu litajitosheleza kimahitaji.
Hivyo, watumishi wa umma tunapaswa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, vilevile tunapaswa kuonyesha tunaheshimu kazi na wajibu wetu.

Imetolewa na Kamati ya Uadilifu ya WHVUM
Share:

0 comments:

Post a Comment