Wednesday 31 December 2014

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 Haijabadilika (Tangazo Toka NECTA)

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015 HAIJABADILIKA

Baadhi  ya  watu  wamekuwa  wakitumiana  ujumbe  kwenye  mitandao  ya  kijamii  wenye kupotosha kwamba    Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  ametangaza kuwa    Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika kuanzia  tarehe  2  hadi  25  Machi  2015  badala  ya   tarehe  4  hadi  27  Mei  2015. 
Aidha,  ujumbe huo  umetoa  sababu  kuu ya mabadiliko  ya ratiba ya  mtihani  kuwa  inatokana  na  mwingiliano  wa  ratiba  ya  Uchaguzi  Mkuu  wa mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Baraza  la  Mitihani  la  Tanzania  linapenda  kuwafahamisha  watahiniwa  wa Mtihani wa Kidato cha Sita  2015 na umma  kwa ujumla  kuwa taarifa  hizo  ni za  UONGO  na  zinalenga  kuupotosha  umma  wa  watanzania. 
  Baraza linapenda  kusisitiza  kuwa  ratiba  ya  Mtihani  wa  Kidato  cha  Sita  2015  HAIJABADILIKA  na  kwamba  Mtihani  huo  utafanyika  kuanzia  tarehe  4 hadi  27  Mei  2015  kama  ilivyopangwa  awali,  Baraza  la Mitihani  linaomba wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.

Imetolewa na,

AFISA HABARI NA UHUSIANO


>>Source

Share:

0 comments:

Post a Comment