Saturday 31 January 2015

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA PILI MWAKA 2014

Title Image

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA PILI MWAKA 2014

news phpto
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali akiwa na Viongozi wengine wa Wizara akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kidato cha pili mwaka 2014 mbele ya Waandishi wa Habari

Mtihani wa Taifa wa darasa la saba ulifanyika tarehe 27/11/2014 na 29/11/2014 na ule wa kidato cha pili ulifanyika tarehe 01/12/2014 – 11/12/2014
Mwaka 2014 mtihani wa kidato cha pili ulishirikisha skuli binafsi na zile zenye michepuo.

MTIHANI WA DARASA LA SABA

•Wanafunzi walioandikishwa walikuwa 27,486 kati yao wanawake ni 14,297 na wanaume 13,189.
•Wanafunzi waliofanya mtihani 25,749 ni sawa na asilimia 93.7 ya wanafunzi walioandikishwa. Wanawake walikuwa 13,662 sawa na asilimia 95.6 na wanaume 12,087, sawa na asilimia 91.7.
•Wanafunzi 18,915 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa masomo ya sekondari. Wanawake ni 10,618 na wanaume ni 8297 sawa na asilimia 73.5. Hii ni upungufu wa asilimia 4.3 ukilinganisha na mwaka uliopita 2013.
•Wanafunzi 105 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia madarasa ya vipawa kati yao wanawake 53 na wanaume 52. Kutoka Unguja ni 84 wanawake 46 na wanaume 38 kutoka Pemba 21 wanawake 07 na wanaume 14. Hili ni ongezeko la asilimia 15.4 ukilinganisha na mwaka uliopita.
•Wanafunzi 1,558 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia madarasa ya michepuo kati yao wanawake 790 wanaume 768, kutoka Unguja 1,105 wanawake 606 na wanaume 449 na kutoka Pemba ni 453 wanawake 184 na wanaume 269. Hili ni ongezeko la asilimia 15.7 ukilinganisha na mwaka uliopita.

SKULI BORA KWA JUMLA DARASA LA SABA

Kwa mwaka 2014 skuli zenye wastani mkubwa ukilinganisha na nyengine
1. Ali Khamis Camp. - Wilaya ya Chake chake.
2. Kibweni - Wilaya ya Magharibi.
3. Kinduni - Wilaya ya Kaskazini ‘B’

SKULI ZILIZOFANYA VIBAYA ZAIDI

1. Mwambe Shamiani - Wilaya ya Mkoani
2. Kigomani - Wilaya ya Kaskazini ‘A’
3. Birikau - Wilaya ya Chake Chake

MITIHANI WA KIDATO CHA PILI

•Wanafunzi 23264 waliandikishwa kufanya mtihani wa kidato cha pili, kati yao wanawake ni 12,431 na wanaume 10,833.
•Wanafunzi 21,944 waliofanya mtihani kati yao 11,825 wanawake na 10,119 wanaume. Hii ni sawa na asilimia 94.3 ya walioandikishwa.
•Wanafunzi 14,384 kati yao wanawake 8,011 na wanaume 6,373 wamefaulu. Na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tatu (Form III). Hii ni sawa na asilimia 65.6. Hili ni ongezeko la asilimia 6.2 ukilinganisha na mwaka uliopita.
Kwa jumla ufaulu wa wanawake ni asilimia 67.8 na ule wa wanaume ni 63.0. Hii inaonesha ufaulu wa wanawake ni mkubwa ukilinganisha na wanaume.

SKULI BORA KWA JUMLA KIDATO CHA PILI

Kwa mwaka 2014 skuli hizo ni hizi zifuatazo:
Skuli zenye wanafunzi 45 na zaidi
1.Zanzibar Commercial.
2.Mikindani Dole
3.Ben Bella
Skuli zenye wanafunzi chini ya 45
1.Feza
2.Kengeja Ufundi
3.Madungu

SKULI ZILIZOFANYA VIBAYA

Skuli zenye wanafunzi 45 na zaidi
1.Connecting Continent
2.Kiwani
3.Wambaa
Skuli zenye wanafunzi chini ya 45
1.Wete Islamic
2.Al-huda
3.Amini Islamic

KESI ZA UDANGANYIFU

Kwa mwaka 2014 kesi ya udanyanyifu ni 2 tu huu upunfufu mkubwa ukilinganisha na mwaka uliopita. Mwaka 2013 kasi za udanyanyifu zilikuwa 5.

WANAFUNZI BORA KITAIFA:

1. DARASA LA SABA:

1.YUSSUF HAMAD RAJAB - MITIULAYA
2.KHADIJA RAJAB SAID - M/KWEREKWE ‘B’
3.THABI KHAMIS KHAMIS - MTOPEPO ‘A’

 2. KIDATO CHA PILI

1.SUMAIYA OMAR MUSSA - FEZA
2.SULEIMAN SALUM MASOUD - MADUNGU
3.KHALID RAJABU JUMA - MBARALI
Share:

0 comments:

Post a Comment