Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi limechagua waombaji 2,543 (Me 1,651 na Ke 892) kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Awamu ya Pili ya Mwaka wa Masomo 2014/2015. Waombaji 1,968 (Me 1226, Ke 742) wamechaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa wanachuo (Central Admission System – CAS) na waombaji 575 (Me 425,Ke 150) wamechaguliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Majina ya waliochaguliwa yamewekwa kwenye tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) na yametumwa kwa wakuu wote wa vyuo na maafisa elimu wa mikoa na wilaya. Waombaji wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ualimu vya Butimba, Tabora, Tukuyu, Mpwapwa, Kinampanda, Mhonda, Nachingwea, Singachini na Tandala. Vyuo vingine ni Tarime, Bustani, Marangu, Morogoro, Klerru na Songea. Mafunzo ya Ualimu yataanza tarehe 01/06/2015 au la kama ilivyoelezwa kwenye fomu za maelekezo za chuo husika, hivyo wanachuo wanatakiwa kuanza kuripoti vyuoni kuanzia tarehe 28/05/2015. Fomu za Maelekezo ya Mafunzo (Joining Instructions) yameambatishwa. Pamoja na maelekezo yaliyopo kwenye fomu za kila chuo, mwanachuo anatakiwa kuripoti chuoni akiwa na vyeti halisi vya masomo na kwa ajili ya taratibu za usajili. Mwombaji yeyote aliyechaguliwa ambaye chuo chake si miongoni mwa vyuo vilivyotajwa lakini ni chuo cha serikali ataweza kuomba uhamisho kwenye vyuo tajwa kwa kuandika barua au kupiga simu 0768 614045 la sivyo atajiunga na masomo mwezi Septemba 2015. Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni tarehe 25 Mei 2015 |
ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA UALIMU (NACTE).
.
IMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAREHE 15/05/2015
0 comments:
Post a Comment