Friday 3 June 2016

MGOGORO BAINA YA UONGOZI NA WANAFUNZI WA MWAKA WA TATU WA SHAHADA YA UDAKTARI KATIKA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI CHA MTAKATIFU FRANCIS (SFUCHAS), IFAKARA


Image result for tcu tanzania

TAARIFA KWA UMMA 

MGOGORO BAINA YA UONGOZI NA WANAFUNZI WA MWAKA WA TATU WA SHAHADA YA UDAKTARI KATIKA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI CHA MTAKATIFU FRANCIS (SFUCHAS), IFAKARA 


1. Tunapenda kuuarifu umma kwamba, Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Mtakatifu Francis ni miongoni mwa Vyuo Vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.

 3. Hivi karibuni Tume ilipokea taarifa ya kuwepo kwa mgogoro baina ya Uongozi wa Chuo na Wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya udaktari wa binadamu (MD3). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiini cha mgogoro huo ni kuwepo kwa dosari katika matokeo ya mitihani ya muhula wa tano (end of semester 5 examinations), ambao hatimaye ulisababisha wanafunzi wote wa mwaka wa tatu kufukuzwa chuoni.

 4. Ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo, Tume imechukua hatua zifutazo:
 a) Imewasiliana na Uongozi wa Chuo na kuuagiza stahiki kupitia upya uamuzi wa kufukuza wanafunzi hao kwa kuzingatia sheria zilizopo ili kutenda haki na kuondoa migogoro. b) Imeunda Timu ya Wataalam kwenda kuchunguza kiini cha mgogoro huo na kubainisha ukweli kuhusu tukio hili kwa lengo la kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

5. Kwa taarifa hii, Tume inawaomba wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Francis popote pale walipo, kuendelea kuwa watulivu wakati huu ambapo suala lao linashughulikiwa na Chuo na Tume.

 Imetolewa na:
PROF. ELEUTHER MWAGENI 
Kaimu Katibu Mtendaji
 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
 31 Mei 2016
Share:

0 comments:

Post a Comment