Tuesday 29 May 2018

JKT : Tarehe ya mwisho kuripoti makambini Vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017



 TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linautangazia Umma mabadiliko ya tarehe ya mwisho kuripoti makambini Vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017 na kuchaguliwa kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria mwaka 2017.

Tarehe ya mwisho kwa vijana hao kuripoti makambini imesogezwa mbele hadi tarehe 09 June 2017.

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu. Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwenzie.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 30 Mei 2017

Share:

0 comments:

Post a Comment