Wednesday 12 June 2019

NACTE : TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA KUTHIBITISHA NA KUBADILI KOZI/CHUO

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

The National Council for Technical Education (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA
KUTHIBITISHA NA KUBADILI KOZI/CHUO

Baraza linapenda kuwafahamisha wanafunzi waliochaguliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na umma kwa ujumla kuwa  Mfumo wa Kuthibitisha (Confirm) kukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa  na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) umefunguliwa rasmi kuanzia  tarehe 9 Juni, 2019 hadi 30 Agosti, 2019. 

Wanafunzi wote waliochaguliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na wanapenda kujiunga na vyuo walivyopangiwa au wanataka kufanya mabadiliko ya vyuo au  kozi wanawajibika kufanya uthibitisho ili kukubali kuchaguliwa kwenye kozi na vyuo walivyopangiwa kupitia kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ambayo ni 
www.nacte.go.tz. 

Kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, mwanafunzi atakayeshindwa kuthibitisha atakuwa amepoteza nafasi yake na hivyo nafasi yake hiyo itachukuliwa na mwanafunzi mwingine kati ya wanafunzi wanaoendelea kuomba kujiunga na vyuo hivyo. 

Aidha, Baraza linawafahamisha wanafunzi wote wanaotaka kufanya mabadiliko ya kozi au vyuo walikochaguliwa, kwamba wataweza kufanya hivyo kuanzia tarehe 10 hadi 30 Agosti, 2019 kupitia tovuti ya NACTE iwapo tu watakuwa wameshathibitisha kukubali kujiunga na vyuo na kozi walizochaguliwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 09/06/2019
Share:

0 comments:

Post a Comment