Wednesday, 28 May 2014

MADARAJA NA GRADE MPYA (BRN)

 

BARAZALAMITIHANI LA TANZANIA

MWONGOZO WAMATUMIZI YA VIWANGO VYA UFAULU

NA UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA KIDATO

CHA NNE NA KIDATO CHA SITA




1.0  UTANGULIZI

Ipo  mifumo  anuwai  inayotumiwa  na  Nchi  mbalimbali  duniani katika kupanga viwango vya ufaulu kwa ajili ya kutunuku vyeti kwa watahiniwa waliofanya mitihani ya Taifa. Hata hivyo, mfumo wenye kutumia Viwango vya  Ufaulu  vinavyobadilika  (Flexible  Grade  Ranges)  na  Viwango vya
Ufaulu  visivyobadilika  (Fixed  Grade  Ranges)  hutumika  zaidi ikilinganishwa  na  mifumo  mingine. Upangaji  wa  viwango  katika Nchi zinazotumia  mfumo  wa  viwango  vinavyobadilika  hutegemea  jinsi watahiniwa  walivyofaulu somo  husika.  Katika  mfumo  huo,  viwango  vya ufaulu  huweza  kutofautiana  baina  ya  somo  na  somo  na  kati  ya  mwaka  mmoja na mwingine kwa sababu kiwango cha ufaulu hutofautiana baina  ya somo moja na jingine. Aidha, kwa nchi zinazotumia mfumo wa viwango vya  ufaulu  visivyobadilika  (Fixed  Grade Ranges),  viwango  vya  ufaulu  vinavyofanana hupangwa  ili  vitumike  kama  kipimo  cha  ufaulu kwa masomo yote kwa kila mwaka.
Tanzania ilikuwa ikitumia mfumo wa viwango vya ufaulu vinavyobadilika (Flexible  Grade  Ranges) kuanzia  mwaka 1973  hadi  2011.  Hata  hivyo, kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne 2012, Baraza la Mitihani la Tanzanialiliamua kuanza  kutumia mfumo  wa  Viwango  vya  Ufaulu  visivyobadilika
(Fixed Grade  Ranges) kwa  madhumuni  ya  kuwawezesha  wadau  kujua viwango  vya  ufaulu  vinavyotumika  katika  kutunuku  matokeo ya  Mitihani ya Taifa.
Baraza la  Mitihani  limeandaa Mwongozo huu ili  kuwawezesha  wadau mbalimbali  wa  elimu  kufahamu  viwango  vya  ufaulu  vilivyoidhinishwa kutumika  katika  Mitihani  ya  Kidato  cha  Nne  na Kidato cha  Sita.  Aidha, mwongozo  huu  umebainisha utaratibu unaotumika  katika  kutunuku
matokeo ya  mitihani  hiyo  kwa  lengo  la kuwawezesha  wadau  wa  elimu kuongeza chachu katika  ufundishaji na ujifunzaji ili  kufikia viwango vya juu vya ufaulu vilivyobainishwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Sehemu  ya  pili ya  Mwongozo  huu inafafanua  malengo  ya  Mitihani  ya Kidato  cha  Nne  na  Kidato  cha  Sita.  Aidha, sehemu  ya  tatu  inafafanua utaratibu  wa kutunuku viwango  vya  ufaulu      na sehemu  ya nne  ni hitimisho.

2.0  MALENGO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE (CSEE) NA KIDATO

CHA SITA (ACSEE)

Malengo ya Mitihani wa Kidato  cha  Nne na Kidato cha  Sita ni  kupima maarifa, ujuzi  na  stadi  alizopata  mtahiniwa za  kumwezesha  kumudu mahitaji ya sayansi na teknolojia katika kujitegemea, ikiwa ni pamoja na  kutimiza  mahitaji  ya    matakwa  ya  jamii  pamoja  na  mazingira  yanayomzunguka. Aidha, matokeo  ya mitihani  hii huwezesha  mamlaka mbalimbali za elimu kuchagua watahiniwa kuendelea na masomo katika  ngazi inayofuata  ikiwa  ni  pamoja  na elimu  ya juu na fani  mbalimbali  za  masomo ya Utalaamu wa Kazi.
Ili  kupata  maarifa  na  ujuzi  unaotakiwa  katika  ngazi  ya  Kidato  cha  Nne, mtahiniwa  wa  shule  (school  candidate)  anatakiwa  kufanya masomo  yasiyopungua saba na yasiyozidi kumi. Kwa upande wa Kidato cha Sita, mtahiniwa  anatakiwa  kufanya  masomo  yasiyopungua manne  ambayo
miongoni  mwake  yapo  masomo  matatu  ya  tahasusi.  Mtahiniwa  wa  Kujitegemea wa Kidato cha Nne anayefanya mtihani kwa mara ya kwanza  anatakiwa kufanya masomo yasiyopungua matatu. Aidha, kwa mtaihiniwa wa  kidato  cha  sita  anayefanya  mtihani  kwa  mara  ya  kwanza  anatakiwa
kufanya masomo yasiyopungua mawili likiwemo somo la General Studies.

3.0  VIWANGO VYA UFAULU NA UTARATIBU WA KUTUNUKU

3.1  Viwango vya Ufaulu

Katika kutunuku  vyeti, Baraza  hutumia  gredi  A,  B+, B, C,  D,  E  na  F ili
kupambanua ufaulu kwa kila mtahiniwa katika Mitihani ya Kidato cha Nne
na Kidato cha Sita. Mchanganuo wa Viwango vya ufaulu vinavyotumika ni
kama inavyoonekana katika Jedwali la 1.

Jedwali la 1: 

Viwango vya Ufaulu katika CSEE na  ACSEE:

GREDI               MFIKO WA             MAELEZO
                             ALAMA
   A                        75-100              Bora sana (Excellent)
   B+                      60-74                Vizuri sana (Very Good)
   B                        50-59                Vizuri  (Good)
   C                        40-49                Wastani (Average)
   D                        30-39                Inaridhisha (Satisfactory)
   E                        20-29                Hairidhishi (Unsatisfactory)
   F                         0-19                  Feli (Fail)

Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata angalau gredi D (alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu  cha ufaulu katika somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu  (Pass) katika somo ni Gredi D. Ufaulu katika Gredi A, B+, B na C utakuwa
ni “Credit Pass” kwa CSEE ambapo kwa ACSEE itakuwa ni “Principal Pass”.

3.2  Matumizi ya Alama Endelevu (CA) katika Alama ya Mwisho

Wakati  wa kupanga  viwango  vya  ufaulu  kama  ilivyoainishwa  katika Jedwali  la  1,  uwiano  wa  alama 30:70 hutumika kukokotoa  Alama  ya  Mwisho  (Final  Score);  ambapo  asilimia   30  ni mchango  wa Alama  Endelevu (CA) na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa  (FE). Katika  Mtihani wa  Kidato  cha  Nne  2013  na Kidato  cha  Sita 2014 mchanganuo wa alama 30 za CA  ni kama inavyoonekana katika Jedwali  la 2 na 3.

Jedwali la 2: Mchanganuo wa CA katika CSEE 

Na.  Aina ya Mtihani                                Alama
1      Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili        15
2      Matokeo ya Mtihani wa Kidato
        cha Tatu – Muhula I                           
3      Matokeo ya Mtihani wa Kidato            10
        cha Tatu – Muhula II
4      Matokeo ya Mtihani wa Kidato
 _       cha Nne – Muhula I                                
5      Kazi Mradi / Project                             5
        Jumla                                                    30

Jedwali la. 3: Mchanganuo wa CA katika ACSEE

  •  Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Tano Muhula wa I na II itachangia alama 15
  •  Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita Muhula wa I itachangia alama 10
  •  Kazi Mradi / Project  itachangia alama  5
           Jumla:= 30

Hata hivyo, kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Sita 2015, mchango  wa  CA  wa  alama 30 utapatikana  kutokana  na  mitihani mbalimbali kama ilivyoaninishwa katika Jedwali la 4 na 5.

Jedwali la. 4: Mchanganuo wa  CA katika  CSEE

  •     Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili itachangia alama  10
  •     Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Tatu – Muhula I  na                                                               Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Tatu – Muhula II itachangia alama 15
  •     Matokeo ya Mtihani  Mock wa Kidato cha Nne itachangia alama 10
  •     Kazi Mradi / Project itachangia alama  5
              Jumla  30

Jedwali la 5:  Mchanganuo wa CA katika  ACSEE

  •   Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Tano Muhula wa I na II itachangia alama 15
  •   Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita Muhula wa I itachangia alama  10
  •   Kazi Mradi / Project itachangia alama  5
             Jumla  30

Muhimu: Katika  somo  ambalo  mtahiniwa hakufanyia Kazi  Mradi, alama za matokeo ya Mitihani ya Mock ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita itachangia alama 15 badala ya 10 zilizoainishwa katika Jedwali la 4 na 5..

3.3  Utaratibu wa Kutunuku Alama ya Mwisho (Final Score)

Ili kupata Alama ya Mwisho (Final Score), Baraza la Mitihani hukokotoa  Alama ya Mwisho kwa kutumia kanuni ifuatayo:

 CFM =   ∂1*FEcm + ∂2*CAcm

Ambapo;
CFM   - Alama ya Mwisho ya Mtahiniwa
∂1   - Uwiano wa Alama katika FE
∂2   - Uwiano wa Alama katika CA
FEcm   - Alama ya Mtahiniwa katika FE (Candidate’s Mark)
CAcm   - Alama ya Mtahiniwa katika CA (Candidate’s Mark)

Mfano: Iwapo katika somo la Geography mtahiniwa amepata alama 13 katika Mtihani wa Mwisho (Final Examination-FE) na Alama Endelevu  zilizooneshwa katika Jedwali lifuatalo:

Kidato cha II alipata alama 89
Mitihani ya Darasani:
  •   Kidato cha III Muhulawa  1 alipata 92
  •   Kidato cha III Muhula wa 2 alipata 93
  •   Kidato cha IV Muhula wa 1 alipata 95
  •   Kazi ya miradi alipata 68

Ukokotoaji wa alama ya mwisho ya mtahiniwa huyu hufanywa kama ifuatavyo:
(a) Mchango wa Mtihani wa Kidato cha Pili katika CA ni:
                                     (15/30) x 89= 45.5

(b) Mchango wa Mitihani ya Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne katika CA ni
                (i)  Wastani wa  alama za Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne   ni
                                     (92 +93+95)/3 = 93.3
               (ii)   Hivyo, mchango wa CA  katika Kidato cha Tatu na Kidato cha
                       Nne ni
                                     (10/30)x93.3 = 31.1
(c) Mchango wa  alama za Kazi-Mradi utakuwa ni
                                      5/30x68 = 11.3

  Hivyo jumla ya alama za CA    
                                   45.5 + 31.1 + 11.3= 87.9  
Kwa kutumia Kanuni CFM = ∂1*FEcm + ∂2*CAcm   na uwiano wa 30:70 
Alama ya Mwisho (CFM) ya mtahiniwa huyu ni
CFM = 70/100x13 + 30/100x87.9 ambayo itakuwa ni 35.
Kwa  Alama 35,  mtahiniwa huyu  atatunukiwa  gredi D ya  ufaulu  katika  somo la
Geography.

3.4  Madaraja ya Ufaulu

Baraza  la  Mitihani  la  Tanzania  hupanga  ufaulu  katika  madaraja mbalimbali.  Madaraja hayo hupangwa kwa kutumia mfumo wa Pointi  au mfumo  wa   Grade  Point  Average  (GPA).  Katika  mfumo  wa  Pointi, mtahiniwa  wa   Kidato  cha  Nne  hukokotolewa  idadi  ya pointi   zake  alizopata katika masomo saba  aliyofanya vizuri na mtahiniwa wa Kidato  cha Sita hukokotolewa  idadi ya pointi  katika masomo matatu ya tahasusi  (combination) aliyojisajili. Katika mfumo wa GPA, jumla ya pointi alizopata  mtahiniwa wa  Kidato  cha  Nne katika  masomo  saba  aliyofanya  vizuri  hugawanywa kwa saba Ili kupata wastani wa pointi alizopata mtahiniwa.
Aidha,  kwa  watahiniwa  wa  ACSEE  idadi  ya  pointi  walizopata  katika  masomo  ya  tahasusi  hugawanywa  kwa  tatu  ili  kupata  wastani  wa  pointi  alizopata mtahiniwa katika masomo hayo.

3.4.1   Madaraja katika Mfumo wa Pointi

Madaraja katika mfumo  wa  pointi  hupangwa kuanzia daraja  la  kwanza hadi  la  nne  yaani  ‘Division  One’,  ‘Division  Two’,  ‘Division  Three’ na ‘Division  Four’ .  Aidha,  daraja  la  I-III  hubainishwa  kwa  idadi  ya pointi  alizopata mtahiniwa wakati daraja la nne hubainishwa kwa kutumia kigezo  cha  mtahiniwa  kufaulu  angalau  D  mbili au  angalau C  moja  au  zaidi.
Mchanganuo wa madaraja ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 6.

Jedwali la 6: Muundo wa Madaraja kwa Kutumia Pointi (CSEE)
DARAJA   POINTI/VIGEZO                        POINTI/VIGEZO
                          CSEE                                           ACSEE

I                        7-17                                                3-7
II                        18-24                                            8-9
III                      25-31                                           10-13
IV              Awe na angalau D                      Awe angalau na D 
                  mbili au Credit Pass                   mbili au Principal pass
                  moja isiyopungua C.                   moja isiyopungua C     
O                Aliyepata ufaulu                         Aliyepata ufaulu      
                   chini ya D  mbili                         chini ya D  mbili

Ambapo pointi kwa kila gredi ni kama ifuatavyo:
A = 1, B+ = 2, B = 3, C= 4, D = 5, E = 6 na F = 7 

Mfano:
a)  Kwa mtahiniwa wa CSEE aliyepata matokeo yaliyoainishwa hapa chini  atakuwa  na idadi  ya  pointi  katika  masomo  saba  aliyofaulu vizuri zaidi kama ilivyooneshwa katika Jedwali lifuatalo:

SOMO                             Civ.  Hist.  Geog.  Kisw.  English  Phy.  Chem.  Biol.  Maths
Pointi  GRADE                 A      B+     B+       B           C        C        C         C         E
UZITO WAGREDI            1      2         2         3            4        4          4         4         6

             Idadi ya  Pointi  alizopata  katika  masomo  Saba  aliyofanya vizuri zaidi ni
                                  1 + 2+ 2 + 3 + 4+ 4 + 4 = = 20
                Hivyo,  kwa Pointi 20,  mtahiniwa  anatunukiwa  matokeo
                yenye Division Two.

b)  Kwa  mtahiniwa  wa  ACSEE  aliyepata   matokeo  yaliyoainishwa
     hapa chini atakuwa na idadi ya pointi katika masomo ya tahasusi
     kama ilivyooneshwa katika Jedwali lifuatalo:

MASOMO                         Tahasusi (combination)            Ziada
                                          Phy.  Chem.  Biol.                 BAM  GS
GRADE                              E        B+      A                       D       A
UZITO WA GREDI           6          2        1                        5         1

Idadi  ya  Pointi  alizopata  katika  masomo  ya  tahasusi
(combination subjects) ni 6 + 2+ 1 = 9.

3.4.2   Madaraja katika Mfumo wa GPA

‘Grade  Point  Average’  (GPA)  ni  Mfumo  wa  Kutunuku  ambao  huonesha wastani  wa  pointi  alizopata  mtahiniwa katika  masomo  aliyofaulu  katika mtihani wake. Madaraja katika mfumo wa GPA hupangwa katika utaratibu wa  Distinction, Merit, Credit na Pass  ambapo daraja la Distinction  ni la ufaulu  wa juu  zaidi na daraja  la Pass ni  la  ufaulu  wa  chini. Mtahiniwa hutunukiwa  Gredi  A,  B+,  B,  C,  D,  E  au  F  kutegemeana  na  ufaulu  wake katika somo ambapo uzito wa alama katika gredi A = 5, B+= 4, B = 3,C=2,  D  =  1,  E  =  0.5 na F  =  0. Mtahiniwa  atahesabiwa  kuwa  amefaulu somo endapo atapata Gredi D ambayo ni sawa na uzito wa Pointi 1.
Ukokotoaji  wa  jumla  ya  GPA  ya  mtahiniwa  hufanyika  kwa  kuzingatia masomo ambayo mtahiniwa amefaulu angalau kwa Gredi D na kuendelea (D, C, B, B+ na A). GPA anayopata mtahiniwa hutokana na wastani wa pointi  alizopata katika  masomo  saba  aliyofanya  vizuri zaidi  kwa  Mtihani wa  Kidato  cha  Nne   au  masomo  matatu  ya  tahasusi  kwa   Mtihani  wa Kidato cha Sita. Aidha, GPA ya mtahiniwa huandikwa katika nafasi moja ya Desimali ambapo nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi yaliyokaribu.
 Mfano, mtahiniwa mwenye  GPA  ya  3.15  itakuwa  sawa  na 3.2 na mtahiniwa mwenye GPA ya 3.14 itakuwa sawa na 3.1.
Muundo  wa madaraja  kwa  kutumia  GPA katika  Mitihani  ya  Kidato  cha Nne na cha Sita ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 7.

Jedwali la 7: Muundo wa Madaraja kwa Kutumia GPA
   DARAJA            CSEE          ACSEE
Distinction            3.6-5.0           3.7-5.0
    Merit                 2.6-3.5           3.0-3.6
   Credit                1.6-2.5            1.7-2.9
    Pass                   0.3-1.5           0.7-1.6
    Fail                    0.0-0.2           0.0-0.6

3.4.3   Kanuni ya Ukokotaoji wa GPA

(a)   Kanuni inayotumika kukokotoa GPA ya mtahiniwa katika Mtihani
wa Kidato cha Nne ni
GPA=  (∑p)/n

Ambapo
p = pointi za masomo saba ambayo mtahiniwa kafaulu
vizuri zaidi
n  =  idadi  ya  masomo  saba  ambayo  mtahiniwa  amefanya
vizuri zaidi.

Mfano, Ukokotoaji  wa  GPA  kwa mtahiniwa  wa  CSEE  aliyepata
matokeo yaliyoainishwa hapa chini ni kama ifuatavyo:
SOMO                          Civ.  Hist.  Geog.  Kisw.  English  Phy.  Chem.  Biol.  Maths
GRADE                          A     B+     B+        B           C        C         C       C         E
UZITO WAGREDI         5      4        4           3            2        2          2       2         0.5

(i)  Masomo  saba  ambayo  mtahiniwa  amefaulu  vizuri  ni
             Civics  (A),  History  (B+),  Geograpghy  (B+),  Kiswahili(B),  English  (C),  Physics  (C)                      na  Chemistry  (C)   ambayo yana uzito wa alama 5, 4, 4, 3, 2, 2 na 2.
(ii)  Wastani  wa  pointi  (GPA)  alizopata  mtahiniwa  katika
       masomo saba aliyofaulu vizuri ni
           (5 + 4 + 4 + 3 + 2 +2 + 2)/7 ambayo itakuwa 3.1.
Hivyo, kwa GPA ya 3.1,mtahiniwa huyu hutunukiwa matokeo yenye Daraja laMerit.
(iii)  Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07, ufaulu wake hautakokotolewa kwa kutumia           GPA na badala yake  atafaulu   katika  kiwango  cha  “Pass”  endapo atapata angalau Gredi D               mbili au C moja.

(b) Kanuni  inayotumika  kukokotoa  GPA  ya  mtahiniwa  katika  Mtihani  wa
  Kidato cha Sita ni
 GPA=  (∑p)/n
Ambapo
p= pointi za masomo ya tahasusi (combination subjects)
n = idadi ya masomo ya tahasusi (combination subjects)

Mfano, Ukokotoaji  wa  GPA  kwa mtahiniwa  wa  ACSEE  aliyepata
matokeo yaliyoainishwa hapa chini ni kama ifuatavyo:
MASOMO                        Tahasusi (combination)            Ziada
                                         Phy.  Chem.  Biol.                BAM  GS
GRADE                             E       B+        A                      D      A
UZITO WA GREDI         0.5      4           5                       1       5

(i)  Katika  masomo matatu  ya  tahasusi  (combination subjects) ambayo  mtahiniwa  ameyafanya  amefaulu katika  masomo  mawili  ambayo  ni  Biology  (A)  na Chemistry  (B+)  yenye uzito  wa  alama  5  na  4.
Mtahiniwa  amepata  Gredi  E  katika  somo  la  Physics ambalo  halitajumuishwa  katika  GPA  kwa  kuwa hakulifaulu.
(ii)  Wastani  wa  pointi  (GPA)  alizopata  mtahiniwa utakuwa ni (5 + 4)/3 ambayo ni 3.0. Hivyo, kwa GPA ya 3.0,  mtahiniwa  huyu  hutunukiwa  matokeo  yenye Daraja la Merit.
(iii)  Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 03, ufaulu wake hautakokotolewa kwa kutumia GPA na badala yake atafaulu  katika  kiwango  cha  “Pass”  endapo atapata angalau Gredi D mbili au C moja.

4.0  HITIMISHO

Baraza  la  Mitihani limeandaa  Mwongozo  huu  ili    kuwawezesha wadau kujua viwango vya ufaulu vinavyotumika pamoja na utaratibu wa matumizi ya Alama Endelevu (CA) katika kutunuku matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na  Kidato cha Sita (ACSEE).  
Baraza la Mitihani la Tanzania linaamini kuwa  Mwongozo huu utakuwa ni  chachu  kwa  Wadau  wa  Elimu  hususan Walimu na  Wanafunzi  ya kuongeza  bidii  katika  ufundishaji na  ujifunzaji ili  kufikia  viwango  vya juu  vya ufaulu vilivyoainishwa.

IMETOLEWANA:
BARAZALAMITIHANI LA TANZANIA
S.L.P 2624
DAR ES SALAAM
APRILI, 2014
Share:

0 comments:

Post a Comment