Kufuatia taarifa za uvumi wa kifo cha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mh. Shukuru Kawambwa, ukweli uko hapa
Taarifa hii imetoka kwenye akaunti ya facebook ya Mbunge wa Chalinze
Mh. Ridhiwani Kikwete na inasomeka kama ifuatavyo:
Ndg Watanzania,Wana Bagamoyo na wapenda maendeleo,
kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo
napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya
Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao
umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba
Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza
majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa
usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na
utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment