Wednesday 16 July 2014

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOBADILISHIWA SHULE KIDATO CHA TANO 2014




                                                                   
KUBADILISHA SHULE NA TAHASUSI KWA WANAFUNZI WA
 KIDATO CHA TANO 2014
Taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha Tano katika Shule za Serikali na
Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 ilitangazwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI mwezi Juni,
 2014. Wanafunzi waliochaguliwa awali walitakiwa kuripoti kuanzia tarehe 10 – 30/7/2014 .
Baada ya taarifa ya Uchaguzi wa wanafunzi kutolewa, baadhi ya wanafunzi/wazazi/walezi
wamewasilisha barua za maombi ya kuwabadilishia wanafunzi waliochaguliwa shule na tahasusi au
 mojawapo ya hivyo. Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupokea imechambua maombi
hayo na kubaini kuwa sababu zilizotolewa kwenye baadhi ya maombi hayo zina tija na hivyo
kulazimika kuridhia kuwabadilishia shule, tahasusi au vyote kwa pamoja baadhi ya wanafunzi hao.
Hata hivyo, haikuwa rahisi kuwabadilishia wanafunzi wote kulingana na uwasilishaji wa maombi yao
 kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye shule na baadhi ya wanafunzi kukosa sifa za kubadilishiwa
 tahasusi kulingana na ufaulu walioupata. Kati ya maombi 3478 yaliyopokelewa na kuchambuliwa,
 wanafunzi 1518 (wavulana 759 na wasichana 759) maombi yao yamekubaliwa na kubadilishiwa shule,
 tahasusi au vyote kwa pamoja. Aidha, wanafunzi ambao hawataona majina yao wafahamu kuwa
maombi yao hayakufanikiwa, hivyo wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa awali.
Hali kadhalika OWM – TAMISEMI inawatangazia wanafunzi 320 wakiwemo wasichana 145 na
wavulana 175 kuwa wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za kidato cha tano, hali iliyotokana
 na kuongezeka kwa nafasi katika baadhi ya shule.
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inaendelea kutoa shukrani kwa ushirikiano wa wadau wa elimu
 na inaendelea kuwasihi waendelee kutoa ushirikiano zaidi kwa ajili ya kuboresha elimu nchini.
Lengo ni moja la kufikia ufaulu wa asilimia 70 au zaidi kwa kidato cha nne wanaohitimu mwaka
 2014 katika kufanikisha malengo ya BRN tuliyojiweka.
Aidha, naendelea kuwakumbusha jukumu tulilonalo la kuongeza shule za sekondari za A – Level
hususani zenye miundombinu ya masomo ya sayansi ili kupata nafasi nyingi zaidi kwa ajili
ya kuwawezesha wanafunzi wote watakaofaulu kuingia kidato cha tano mwaka 2015, wanapatiwa
nafasi.
Aidha, wanafunzi wote ambao maombi yao yamekubaliwa wanatakiwa kuripoti shuleni si
 zaidi ya tarehe 30/7/2014 kama ilivyotangazwa awali.


MAJINA YA WANAFUNZI WALIOBADILISHIWA SHULE KIDATO CHA TANO 2014:  

1.  MABADILIKO YA FORM V SELECTION (2014/2015) KWA WASICHANA pdf

2. MABADILIKO YA FORM V SELECTION (2014/2015) KWA WAVULANA pdf

 
Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI
JULAI, 2014

Share:

0 comments:

Post a Comment