Tuesday 22 July 2014

ORODHA MPYA NA MABADILIKO YA SHULE - FORM V 2014

                                              JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                                          OFISI YA WAZIRI MKUU
                                         TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KUBADILISHA SHULE NA TAHASUSI WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2014:

Ofisi  ya  Waziri  Mkuu  –  TAMISEMI  imefanya  marekebisho  ya  shule  na tahasusi baadaya kupokea maombi ya baadhi ya wazazi na walezi kuhusu kufanya  mabadiliko  husika.   Mabadiliko  hayo  yamefanyika  baada  ya kuona hoja zilizotolewa zina tija.

Aidha, wanafunzi ambao  maombi yao yamekubaliwa wanatakiwa kuripoti shuleni si zaidi ya tarehe 30/07/2014 kama ilivyotangazwa awali.Mabadiliko haya ni ya pili na ya mwisho.

Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI
21 JULAI, 2014 


TAARIFA KAMILI:
 
KUBADILISHA SHULE NA TAHASUSI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2014
Taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha Tano katika Shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 ilitangazwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI mwezi Juni, 2014. Wanafunzi waliochaguliwa awali walitakiwa kuripoti kuanzia tarehe 10 – 30/7/2014 .
Baada ya taarifa ya Uchaguzi wa wanafunzi kutolewa, baadhi ya wanafunzi/wazazi/walezi wamewasilisha barua za maombi ya kuwabadilishia wanafunzi waliochaguliwa shule na tahasusi au mojawapo ya hivyo. Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupokea imechambua maombi hayo na kubaini kuwa sababu zilizotolewa kwenye baadhi ya maombi hayo zina tija na hivyo kulazimika kuridhia kuwabadilishia shule, tahasusi au vyote kwa pamoja baadhi ya wanafunzi hao.
Hata hivyo, haikuwa rahisi kuwabadilishia wanafunzi wote kulingana na uwasilishaji wa maombi yao kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye shule na baadhi ya wanafunzi kukosa sifa za kubadilishiwa tahasusi kulingana na ufaulu walioupata. Kati ya maombi 3478 yaliyopokelewa na kuchambuliwa, wanafunzi 1518 (wavulana 759 na wasichana 759) maombi yao yamekubaliwa na kubadilishiwa shule, tahasusi au vyote kwa pamoja. Aidha, wanafunzi ambao hawataona majina yao wafahamu kuwa maombi yao hayakufanikiwa, hivyo wanatakiwa kuripoti kwenye shule walizopangiwa awali.
Hali kadhalika OWM – TAMISEMI inawatangazia wanafunzi 320 wakiwemo wasichana 145 na wavulana 175 kuwa wamechaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za kidato cha tano, hali iliyotokana na kuongezeka kwa nafasi katika baadhi ya shule.
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inaendelea kutoa shukrani kwa ushirikiano wa wadau wa elimu na inaendelea kuwasihi waendelee kutoa ushirikiano zaidi kwa ajili ya kuboresha elimu nchini. Lengo ni moja la kufikia ufaulu wa asilimia 70 au zaidi kwa kidato cha nne wanaohitimu mwaka 2014 katika kufanikisha malengo ya BRN tuliyojiweka. Aidha, naendelea kuwakumbusha jukumu tulilonalo la kuongeza shule za sekondari za A – Level hususani zenye miundombinu ya masomo ya sayansi ili kupata nafasi nyingi zaidi kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wote watakaofaulu kuingia kidato cha tano mwaka 2015, wanapatiwa nafasi.
Aidha, wanafunzi wote ambao maombi yao yamekubaliwa wanatakiwa kuripoti shuleni si zaidi ya tarehe 30/7/2014 kama ilivyotangazwa awali. 


ORODHA MPYA NA MABADILIKO YA SHULE - FORM V 

1. ORODHA YA WANAFUNZI WASICHANA WALIOCHAGULIWA BAADA YA NAFASI KUONGEZEKA

2. ORODHA YA WANAFUNZI WAVULANA WALIOCHAGULIWA BAADA YA NAFASI KUONGEZEKA

3. ORODHA YA WANAFUNZI WASICHANA WALIOBADILISHIWA SHULE KIDATO CHA TANO 2014 - AWAMU YA PILI NA YA MWISHO

4. ORODHA YA WANAFUNZI WAVULANA WALIOBADILISHIWA SHULE KIDATO CHA TANO 2014 - AWAMU YA PILI NA YA MWISHO
 
Imetolewa na Katibu Mkuu
OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI
JULAI, 2014
Share:

0 comments:

Post a Comment