Thursday, 14 August 2014

Gazeti la sani laonywa kwa kuwapa hofu wananchi

SERIKALI imelionya gazeti la SANI kwa kuchapisha habari na pichazisizokuwa za kweli na kuzua hofu kwa wananchi.
Hatua hiyo inafuatia na gazeti hilo kuchapisha habari zilizokuwa na kichwa kisemacho EBOLA YATUA na kuonyesha picha za maiti bila kueleza kuwa sio za tukio lililotokea nchini.
Onyo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene wakati akiongea na waandishi wa habari.
“Sio vizuri na kuleta mizaha katika habari makini na zinazogusa maisha ya wananchi kama ugonjwa wa EBOLA kwa unasababisha hofu miongoni mwa jamii” amesema Mwambene.
Amesema kuwa hadi hivi sasa hakuna mgonjwa yoyote aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hapa nchini na wala haujafika.
Hata hivyo Mwambene ameongeza kuwa pamoja na kutokuwa na mgonjwa yoyote hapa nchini, Serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaripotiwa kuingia nchini.
Ametaja hatua hizo ni Kutenga vituo maalum vya kuwapima wagonjwa watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo katika viwanja vya ndege na sehemu zote za kuingilia nchini.
Share:

0 comments:

Post a Comment