Usalama wa Raia Kwanza
HAKI NA WAJIBU WANGU, WAKO NA WETU SOTE.
Kila raia wa Tanzania ana haki ya Usalama wa maisha yake na mali zake na pia kuheshimu mali na maisha ya mtu mwingine.
Ni wajibu wetu sote kuirejea misingi ya kudumisha AMANI na USALAMA kama mtaji namba moja wa Ustawi wa Jamii.
Kumbuka mara zote kutoa taarifa ukiona jambo la kutia Mashaka au jambo lisilo la kawaida katika maeneo ya makazi, maeneo ya biashara na hata maeneo ya ibada. Mbinu ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu inasaidia kuzuia uhalifu na kupambana na uhalifu huo endapo umekwishakutokea.

Tusaidiane
kuzuia uhalifu kwa mbinu ya kutoa taarifa kituo cha Polisi cha karibu
na pia kwa walinzi wa amani wanaotambuliwa kisheria. Kila mtu ana haki
na wajibu wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa afisa wa Polisi au
mtu yeyote mwenye mamlaka katika eneo husika kama vile Mkuu wa Mkoa,
Mkuu wa Wilaya, Hakimu, Wabunge, Viongozi wa Dini na Wenyeviti wa
Serikali za Mitaa.
Tafadhali toa taarifa ya uhalifu na wahalifu kwa kutumia namba za simu za Makamanda wa Polisi wa Mikoa au namba ya simu ya Makao Makuu ya Polisi 0754 78 55 57. Taarifa hizo pia zinaweza zikatolewa kwa njia ya mdomo kwa maana ya kwenda ana kwa ana, kwa maandishi au kupitia ujumbe mfupi wa simu.

FAIDA YA KUTOA TAARIFA YA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA ENEO:
Wahalifu watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Jamii itakuwa salama na kuondokana na matishio ya wahalifu na uhalifu, hivyo, kushiriki ipasavyo katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Mahali pakiwa salama uwekezaji utakuwa na kuwa chanzo cha ajira kwa wananchi husika.
HASARA ZA KUTOTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU:
Jamii kuishi kwa hofu ya kufanyiwa uhalifu, hivyo, kushindwa kushiriki ipasavyo katika masuala ya kimaendeleo.
Kuwepo kwa vikundi vya kuhatarisha amani na utulivu kwa wananchi kama vile ugaidi, ambavyo vinaweza kupata hifadhi ndani ya jamii husika.
Uwekezaji kupungua na kupelekea kupungua wa nafasi za ajira kwa vijana.
TUSHIRIKIANE KATIKA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UHALIFU NA WAHALIFU HAPA NCHINI.
0 comments:
Post a Comment