Friday, 15 August 2014

Kuhusu Kuapishwa kwa Majaji

                                 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
                   DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atawaapisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kesho Ijumaa tarehe 15 Agosti, 2014, katika viwanja vya Ikulu, saa tano kamili asubuhi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie jina la mwandishi na mpigapicha ambao watafika ikulu kwa ajili ya shughuli hii.
Kwa umuhimu wa maandalizi ya shughuli hii, tunaomba majina ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu leo, na mwisho wa kupokea majina hayo ni kesho 15/8/2014 saa tatu kamili asubuhi.
Aidha tunaomba ifikapo saa 4.30 asubuhi wawe wamefika lango kuu la Ikulu
Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika. Aidha, tunasisitiza mavazi yawe nadhifu na heshima, kwa kuwa hii ni shughuli ya Kitaifa.
Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.
Dar es Salaam.
14 Agosti, 2014
Share:

0 comments:

Post a Comment