Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wakazi wa mkoa wa
Dar es Salaam wenye umri wa miaka 18 na zaidi ambao hawakupata fursa ya
kujiandikisha au kuchukuliwa alama za vidole na picha kufika kwenye
ofisi za NIDA za wilaya kupata huduma hizi. Ofisi hizi katika kila
wilaya ni:-
WILAYA YA ILALA
1. Tabata Shule
2. Gongo la Mboto (Kituo Kipya)
WILAYA YA TEMEKE
1. Chang’ombe bango lipo kituo cha Bora karibu na ofisi za TRA
2. Kigamboni karibu na Msikiti wa Aziza.
WILAYA YA KINONDONI
1. Goig – Mbezi Beach mkabala na Shamo au jengo la Maktech
2. Magomeni jengo la TTCL karibu na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni.
Siku za kutoa huduma: Jumatatu – Jumamosi Saa 02:00 Asubuhi – Saa 09:30 Alasiri.
Imetolewa na;
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
0 comments:
Post a Comment