Wednesday, 13 August 2014

Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.


                                             


Rais  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa Tanzania,  Mheshimiwa  Dkt.  Jakaya Mrisho  Kikwete,  baada  ya  kushauriana  na  Tume  ya  Utumishi  wa  Mahakama, amewateua wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.

WATUMISHI WA MAHAKAMA

(i)    Bw.  Penterine  Muliisa  KENTE,  ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam.
(ii)   Bw. Benedict Bartholomew MWINGWA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
(iii)    Bw.  Edson  James  MKASIMONGWA, ambaye  kabla  ya  uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.
(iv)    Bw.  David  Eliad  MRANGO,  ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Msajili, Baraza la Ushindani, Dar es Salaam.
(v)    Bw.  Mohamed  Rashid  GWAE, ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Msajili, Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam.
(vi)    Dkt.  John  Eudes  RUHANGISA, ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha.
(vii)    Bw.  Firmin  Nyanda  MATOGORO, ambaye  kabla  ya  uteuzi  huu alikuwa Naibu Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam.

MAWAKILI  WA  SERIKALI  NA  TAASISI  MBALIMBALI  ZA SERIKALI

(i)    Dkt.  Eliezer  Mbuki  FELESHI, ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Mkurugenzi wa Mashitaka, Dar es Salaam.
(ii)    Bi.  Barke  Mbaraka  Aboud  SEHEL,  ambaye  kabla  ya  uteuzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
(iii)   Bi. Winfrida Beatrice KOROSSO ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam.
(iv)    Bi.  Lilian  Leonard  MASHAKA, ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Naibu  Mkurugenzi  Mkuu,  Taasisi  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na Rushwa, (TAKUKURU), Dar es Salaam.
(v)    Bi.  Leila  Edith  MGONYA,  ambaye kabla  ya  uteuzi  alikuwa Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.
(vi)    Bw.  Awadhi  MOHAMED,  ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Mchunguzi  Mkuu,  Taasisi  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  Rushwa, (TAKURURU), Dar es Salaam.

MAWAKILI WA KUJITEGEMEA

(i)   Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam.
(ii)    Bw.  Amour  Said  KHAMIS, kutoka  AKSA  Attorneys,  Dar  es Salaam.
(iii)   Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemeana  Mhadhiri  Mwandamizi,  Chuo  Kikuu  Huria,  Dar  es Salaam.
(iv)   Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Wakili wa Kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.
(v)   Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.

WATUMISHI WA VYUO VIKUU

(i)    Dkt.  Mary  Caroline  LEVIRA,  ambaye  kabla  ya  uteuzi  alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha.
(ii)    Dkt. Modesta  Opiyo  MAKOPOLO,  ambaye  kabla  ya  uteuzi alikuwa  Mkuu  wa  Kitivo  cha  Sheria,  Chuo  Kikuu,  Mzumbe, Morogoro.

Wateuliwa  wote  wataapisha tarehe  15  Agosti,  2014  Saa  05.00  asubuhi  katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.

Imetolewa na Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo
13 Agosti, 2014
Share:

0 comments:

Post a Comment