Lorietha Laurence
Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa sekta binafsi kutumia fursa zinazotolewa nchini ili kujifunza aina ya miradi inayoweza kukopesheka.
Hayo yamezungumzwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina ya wafanyabiasahara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Wafanyabiashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA).
Aliongeza kusema kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi na kwa kupitia semina hii itasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha kutokana na mafunzo yanayotolewa.
Naye Rais Mtendaji Mkuu wa Benki ya PTA bw.Admassu Tadesse amefurahishwa na muitikio wa watanzania katika kuhudhuria semina hiyo na utayari wao kutaka kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara .
“Najisikia furaha kuwepo mahali hapa kuweza kushirikiana nanyi katika semina hii kwani najifunza mengi kutoka kwenu kama ambavyo nanyi mnavyojifunza kutoka kwetu na huu ni ushirikiano mzuri wenye kuleta maendeleo “ alisema Tadessa.
Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama ikiwa na lengo la kuwa Taasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini mwa Afrika katika utoaji wa huduma za kibenki ambapo
mwaka huu imetimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1985.
0 comments:
Post a Comment