Tuesday, 26 August 2014

Real Madrid kujenga Soka Aakademi Tanzania

 

 
SERIKALI ya Tanzania inatarajia kujenga Akademia ya michezo yenye nembo ya Real Madrid
ya nchini Hispania ikiwa ni njia ya kuwapa vijana fursa ya kujifunza michezo hasa mpira
wa miguu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Fenella Mukangara (MB) wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
katika Hotel ya Ledger Plaza (Bahari Beach) nakujumuisha wachezaji wa zamani wa Real
Madrid pamoja na zaidi ya watoto yatima 2000.
Waziri Fenella amesema kuwa ujumbe wa Real Madrid umeonesha nia ya dhati ya kujenga
Akademi hiyo ya michezo ambayo itakuwa ni ya kwanza kujengwa na Klabu hiyo kongwe
katika ukanda huu wa Afrika.
Aidha Waziri Fenella aliongeza kuwa katika mazungumzo ya awali wataalamu kutoka timu
ya Real Madrid watatoa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa Soka akiaminiwa kuwa mafunzo
hayo yatawaongezea ufanisi kwa kuwa wakufunzi wao watatoka katika miongoni mwa moja
ya timu bora Duniani.
“Wenzetu wa Real Madrid wameonesha dhamira ya kujenga Soka Akademi hapa nchini
kwetu hivyo nasi kama Serikali tunajipanga katika kufikia makubaliano ili utaratibu wa
ujenzi uanze mara moja na ikiwezekana ukamilike mapema vijana wetu wapate sehemu ya
kujifunzia michezo hasa mchezo wa Soka” Alisema Dkt. Fenella.
Wakati huo huo Mkuu wa Msafara wa wachezaji wa zamani wa Real Madrid Rayco Garcia
amesema kuwa wapo tayari kufungua Akademi hapa nchini Tanzania kwani ni nchi yenye
watu wakarimu,nakueleza kufaha yake ya kufika Afrika kwa mara ya kwanza na Tanzania
ikiwa ndiyo nchi pekee ambayo timu ya Real Madrid imetembelea barani Afrika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TSN Supermarket kampuni ambayo ndiyo iliratibu ujia wa
timu hii Bw. Farough Bangozah amesema kuwa ujio wa wachezaji wa zamani wa Real
Madrid Tanzania imetokana na ahadi iliyoitolewa mwaka 2007 na Rais Jakaya Kikwete
Farough aliongeza kuwa kupitia michezo vijana wanatanufaika kwa kujiepusha na makundi
mabaya hali kadhali michezo ni njia nzuri katika kutangaza biashara pamoja na nchi kwa
ujumla.
Katika ulimwengu huu wa sasa soka imekuwa ni biashara kubwa hivyo ni wajibu wa walezi
na wanajamii Wote kuhakikisha wanaendeleza vipaji vya watoto na siyo kutegemea serikali
peke yake kwani soka inasaidia vijana kuwa na mwenendo mzuri pamoja na uelewa mzuri
pia kuleta maendeleo ya nchi
Wachezaji wa zamani wa Real Madrid walikuja nchini kwa ziara ya siku nne ambapo
waliwasili mnamo tarehe 22 na kucheza mechi ya kirafiki na wachezaji wa zamani wa Taifa
Stars TSN Eleven Stars ambapo mchezo huo ulimalizika huku Real Madrid wakiibuka
washindi kwa jumla ya mabao 3-1. Baaada ya meche wachezaji hao wlifanikiwa kutembelea
mbuga za wanyama za Ngorongoro, Serengeti Kinata na kupanda Mlima Kilimanjaro.
Share:

0 comments:

Post a Comment