Monday, 8 September 2014

Ziara ya Mhe. Yoweri K. Museveni nchini Tanzania



Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

 

Katika ziara hiyo nchini, Mhe. Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.

 

 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Share:

0 comments:

Post a Comment