Akitangaza matokeo ya ufaulu huo kwa vyombo vya habari na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo.
Naibu waziri, Majaliwa amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa wasichana ni 219,996 sawa na asilimia 97.1 na wavulana 218964 sawa na asilimia 97.28 na kuongeza kuwa takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa imeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na 96.3 ya waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka 2013.
Aidha alisema
Wanafunzi 10,331 wamepata alama za daraja A
Wanafunzi 98,789 wamepata alama za daraja B
Wanafunzi 342,272 wamepata daraja C
Wanafunzi 321,939 wamepata daraja D
Wanafunzi 18,787 wamepata daraja E
Alama za juu kwa wavulana ilikuwa 243 na wasichana alama 240 kati ya alama 250.
Amewahimiza wazazi, walezi, na jamii kushirikiana na uongozi wa wilaya, halmashauri, na shule kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, na kuhudhuria hadi watakapomaliza elimu ya sekondari.
Halmashauri zilizobakiza jumla ya wanafunzi 12,432 katika awamu ya Kwanza ni Dodoma, (9,824) Dar es salaam (1,414), Morogogoro (752), Mtwara (281) na Katavi (161). Waziri Majaliwa ameziagiza Halmashauri hizo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi hao kujiunga na Kidato cha Kwanza ifikapo mwezi Machi.
0 comments:
Post a Comment