BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015 HAIJABADILIKA
Baadhi ya watu wamekuwa wakitumiana ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye kupotosha kwamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametangaza kuwa Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 25 Machi 2015 badala ya tarehe 4 hadi 27 Mei 2015.Aidha, ujumbe huo umetoa sababu kuu ya mabadiliko ya ratiba ya mtihani kuwa inatokana na mwingiliano wa ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwafahamisha watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kuupotosha umma wa watanzania.
Baraza linapenda kusisitiza kuwa ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 HAIJABADILIKA na kwamba Mtihani huo utafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 27 Mei 2015 kama ilivyopangwa awali, Baraza la Mitihani linaomba wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
0 comments:
Post a Comment