Friday, 15 January 2016

Taarifa Maalum kwa Wamiliki wa Vyuo kutoka NACTE

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma, na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa siku ya Ijumaa, tarehe 15/01/2016 saa mbili (2:00) asubuhi, kutakuwa na mkutano na wamiliki wote wa vyuo binafsi vyenye usajili wa Baraza, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini katika ofisi za NACTE  makao makuu, Mikocheni-Dar-es-Salaam.

Mkutano huo utaongelea mambo muhimu katika kuboresha sekta ya elimu ya ufundi nchini. Mkutano huo utafunguliwa na Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako (MB), Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Wamiliki/Meneja wote wa vyuo binafsi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za kidini mnaombwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa. Mialiko rasmi ya kimaandishi imeletwa kwenu kupitia TAMONGSO, TAPIE, APHECOT, CSSC na BAKWATA.


Imetolewa na:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment