Tuesday, 9 February 2016

Kufutwa kwa leseni ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa Tanzania (Tanzania International University)

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

Taarifa kwa Umma


Image result for ipp tcu 
 

Tanzania International University

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inapenda kuwataarifu wananchi na umma kwa ujumla kwamba, imefuta leseni ya uanzishwaji wa Chuo Kikuu Cha Kimataifa Tanzania (Tanzania International University), kwa sababu zifuatazo:

1. Kushindwa kutimiza masharti yaliyoainishwa kwenye leseni waliyopewa na Tume;
2. Kukiuka masharti ya ithibati kwa kuanzisha na kufundisha programu za astashahada na stashahada bila ithibati ya mamlaka husika.


Kwa mantiki hiyo, Tume haitambui astashahada na stashahada zote zilizotolewa, zinazotolewa au zitakazotolewa na Chuo hiki. Tume inawataka wananchi kuwa makini na chuo hiki na endapo wakiwa na wasiwasi na uhalali wa chuo chochote wasisite
kuwasiliana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania au mamlaka nyingine zinazohusika ili kupata taarifa sahihi.


Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
8 Februari 2016

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment