Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadaiwa wote waliopo Dar es Salaam kuwa Ofisi za Bodi zitakuwa wazi kwa siku mbili za kesho, Jumamosi, Julai 30, 2016 na Jumapili, Julai 31, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 mchana ili kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuwasiliza wadaiwa.
Hii ni fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kulipa mikopo kupata taarifa kuhusu madeni yao.
Bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wadaiwa wote ambao hawataanza kulipa madeni yao mara moja. Hatua hizo ni pamoja na:
i. Kufikishwa mahakamani;
ii. Kutozwa faini;
iii. Kunyimwa fursa za kupata mikopo;
iv. Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na
v. Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.
i. Kufikishwa mahakamani;
ii. Kutozwa faini;
iii. Kunyimwa fursa za kupata mikopo;
iv. Kunyimwa fursa za masomo nje ya nchi; na
v. Kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.
Nyote mnakaribishwa ili kutumia fursa hii muhimu.
Imetolewa na:
Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P. 76068,
DAR ES SALAAM
Baruapepe: info@heslb.go.tz
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P. 76068,
DAR ES SALAAM
Baruapepe: info@heslb.go.tz
‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’
0 comments:
Post a Comment