TAARIFA KWA UMMA
linawatangazia wanafunzi wote waliohitimu kidato cha
sita mwezi Mei 2016, ambao hawakuchaguliwa
kujiunga na mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria
Operesheni Magufuli Awamu ya Kwanza na
hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya
juu, kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa
kabla ya tarehe 13 Desemba 2016 .
Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linaukumbusha umma
kuwa ni kosa la jinai kwa kijana aliyetangaziwa
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria
kushindwa kujiunga na mafunzo hayo.
Kosa hilo la jinai, ni kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la
Kujenga Taifa, Sura Namba 193 ya mwaka 1964 na
kufanyiwa mapitio mwaka 2002 kifungu cha 11 kifungu
kidogo cha (8).
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mwanafunzi
yeyote atakayeshindwa kuripoti ndani ya muda
uliopangwa wa kuanza mafunzo ya JKT Mujibu wa
Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili mwaka
2016.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 07 Desemba 2016
0 comments:
Post a Comment