BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA
KUTHIBITISHA NA KUBADILI KOZI/CHUO
Baraza linapenda kuwafahamisha wanafunzi waliochaguliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi na umma kwa ujumla kuwa Mfumo wa Kuthibitisha (Confirm) kukubali kujiunga na kozi zinazosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) umefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 9 Juni, 2019 hadi 30 Agosti, 2019.
Wanafunzi wote waliochaguliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na wanapenda kujiunga na vyuo walivyopangiwa au wanataka kufanya mabadiliko ya vyuo au kozi wanawajibika kufanya uthibitisho ili kukubali kuchaguliwa kwenye kozi na vyuo walivyopangiwa kupitia kiunganishi kinachoitwa Uthibitisho TAMISEMI katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ambayo ni
www.nacte.go.tz.
Kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, mwanafunzi atakayeshindwa kuthibitisha atakuwa amepoteza nafasi yake na hivyo nafasi yake hiyo itachukuliwa na mwanafunzi mwingine kati ya wanafunzi wanaoendelea kuomba kujiunga na vyuo hivyo.
Aidha, Baraza linawafahamisha wanafunzi wote wanaotaka kufanya mabadiliko ya kozi au vyuo walikochaguliwa, kwamba wataweza kufanya hivyo kuanzia tarehe 10 hadi 30 Agosti, 2019 kupitia tovuti ya NACTE iwapo tu watakuwa wameshathibitisha kukubali kujiunga na vyuo na kozi walizochaguliwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 09/06/2019
0 comments:
Post a Comment