Tuesday, 28 March 2023

TAMISEMI: KUBADILISHA COMBINATION NA MACHAGUO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE 2022

 Ofisi ya Rais - TAMISEMI imetoa fursa kwa Wahitimu wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne kufanya mabadiliko ya Tahasusi (COMBINATION) na kozi za Vyuo vya Kati walizochagua kupitia fomu za Selform mwaka 2022.

Mabadiliko yanafanyika kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz

Jinsi ya kufanya mabadiliko unatumia namba yako ya mtihani, jina la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulu katika somo au swali utakaloulizwa ambapo zoezi hili limeanza Kufanyika kuanzia tarehe 15/03/2023 na mwisho ni tarehe 06/04/2023.

“Kwa changamoto yoyote, wasiliana nasi kwa barua pepe helpdesk@tamisemi.go.tz au piga 0262 160 210 na 0735 160 210 na ili kujenga uelewa wa pamoja Mzazi/Mlezi unashauriwa kushirikiana na Mtoto wako katika mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi na kozi za Vyuo vya kati”

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment