Wednesday, 12 April 2023

TAMISEMI: AJIRA MPYA WATUMISHI 21,200.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ametoa nafasi za ajira 21,200 katika Kada ya Elimu na Afya ambapo katika Kada ya Elimu ni Watumishi 13,130 watakaofundisha katika Shule za Msingi na Sekondari na katika Kada ya Afya ni Watumishi 8070 watakaofanyakazi katika Hospital za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati.

Tangazo hilo la Serikali limetolewa na Waziri wa TAMISEMI Angella Kairuki leo April 12,2023 Jijini Dodoma ambapo amesema mwisho wa maombi hayo ni tarehe 25 April,2023 saa 05:59 usiku.

“Kwa Kada ya Elimu Waombaji wawe ni wale waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2022 na Afya wawe wasiozidi miaka 45 na wanatakiwa kutuma maombi kuanzia leo tarehe 12,04,2023 na mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2023 saa 05:59 usiku”

Kwa upande wa Watumishi wanaoendelea kujitolea, Waziri Kairuki amesema TAMISEMI ina orodha yao ambapo amesisitiza waombe ajira kupitia tangazo hilo ili wapate nafasi ya kuingia katika mfumo wa ajira za Serikali.


Tangazolaajira Ualimunaafya Tamisemi Aprili 2023 by Daniel Eudes on Scribd

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment