Friday, 26 September 2014

Tangazo Maalum Toka JKT


TANGAZO

MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAKANUSHA HABARI ILIYOTOLEWA NA MTANDAO WA JAMII FORUM KUWA NAFASI ZA VIJANA WA KUJITOLEA ZIMETANGAZWA.
HABARI HIYO IMETUMWA NA MTU ANAYEJIITA MTANZA MWENYE NIA TAREHE 24 SEPTEMBA 2014.
UKWELI NI KWAMBA NAFASI HIZO HAZIJATOLEWA NA TAARIFA HIYO SI SAHIHI, HAKUNA KITU KAMA HICHO.
AIDHA, IFAHAMIKE MATANGAZO YOTE YAHUSUYO JESHI LA KUJENGA TAIFA HUTANGANGAZWA KWENYE TOVUTI YA JKT AMBAYO NI WWW.JKT.GO.TZ . AMA NA MKUU WA JKT KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT TAREHE 25 SEPTEMBA 2014.
Share:

0 comments:

Post a Comment