Saturday, 25 April 2015

Taarifa kwa Umma kuhusu Recruitment Portal

Image result for tanzania emblem
Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma hivi karibuni ilianzisha majaribio ya kupokea maombi kazi kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia ‘Recruitment Portal’ ikiwa ni hatua za majaribio kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mfumo huu hivi karibuni.
Tangu kuanza kwa majaribio ya mfumo huo hivi karibuni, matangazo ya kazi matano (5) yametangazwa na kuwalekeza waombaji kazi kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo huo wenye anuani http://portal.ajira.go.tz  ambapo tathmini inaonyesha kuwa na mafanikio.
Matangazo ya nafasi za kazi ambayo tayari Sekretarieti ya ajira imeyatangaza kupitia mfumo huo yalitangazwa kwa niaba ya Wakala wa Serikali Mtandao(e-GA) la tarehe 22 Aprili, 2014, Tangazo la Mkemia kuu wa Serikali la tarehe 4 Desemba, 2014 na Tangazo la mamlaka ya hali ya hewa(TMA) la tarehe 4 Desemba, 2014 ambayo tayari mchakato wake wa ajira umeshakamilika.
Aidha matangazo ya kazi yaliyobaki ambayo ni tangazo la nafasi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi la tarehe 16 Januari, 2015 taratibu za kuwaita waliofaulu kwa ajili ya usaili zinaendelea. Matangazo mengine mawili yalitangazwa tarehe 10 Machi, 2015 na mchakato wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya ‘Recruitment portal’ unaendelea hadi tarehe 25 Machi, 2015.

Sekretarieti ya ajira imelazimika kutoa ufafanuzi kwa umma kupitia taarifa hii ili kukanusha baadhi ya taarifa zinazosambazwa kuwa utaratibu wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya posta umefungwa rasmi.

Ukweli ni kwamba mchakato wa kupokea maombi ya kazi kwa njia ya posta bado unaendelea na hata sasa baadhi ya matangazo yaliyotangazwa kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz yanahitaji waombaji kutuma maombi yao kupitia posta isipokuwa kwa matangazo tajwa mawili ya tarehe 10 Machi, 2015 ambayo waombaji wameelekezwa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao. Hivyo tunawahimiza waombaji kazi kusoma matangazo hayo kwa umakini kabla ya kutuma maombi yao ya kazi.

Katibu wa Sekretarieti ya ajira anapenda kuwasisitiza wananchi hususani waombaji kazi kuwa ofisi yake inaendelea na uimarishaji wa mfumo mpya wa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao (recruitmemnt portal) ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi hivi karibuni mara baada ya taratibu zote kukamilika na anawasisitiza waombaji kazi waendelee kujisajili katika mfumo huo mpya kwa kuingiza taarifa zao mbalimbali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 17 Machi, 2015.

Attachments:
Download this file (Recruitment Portal User Manual.pdf)How to apply[How to apply]2285 Kb
Share:

0 comments:

Post a Comment