Friday, 1 May 2015

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA MAOMBI KWA NJIA YA MTANDAO KWA STASHAHADA NA ASTASHAHADA ZA AFYA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA MAOMBI KWA NJIA YA MTANDAO KWA STASHAHADA NA ASTASHAHADA ZA AFYA
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi likishirikiana  na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii linataarifu umma kuwa mfumo wa maombi kwa njia ya mtandao uko wazi kwa waombaji wapya kwenye vyuo vya afya kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Sifa za kujiunga:
  1. Stashahada:  Ufaulu wa Fizikia/Sayansi ya Uhandisi – D, Kemia – C, Baiolojia – C kwenye mtihani wa kidato cha IV

  1. Astashahada: Ufaulu wa Fizikia/Sayansi ya Uhandisi – D, Kemia – D, Baiolojia – D kwenye mtihani wa kidato cha IV

  1. Stashahada ya Juu na mafunzo ya kujiendeleza: Ufaulu wa Baiolojia – D kwenye mtihani wa kidato cha IV, mfanyakazi kwa zaidi ya miaka miwili, picha, na cheti na nakala ya matokeo ya astashahada au stashahada pamoja na barua ya mwajiri. Waombaji wa masomo ya Uuguzi waambatanishe leseni ya Uuguzi.

ANGALIZO:
Maombi yote yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili na mwisho wa maombi ni tarehe 18 Julai 2015.

Katibu Mtendaji
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

Share:

0 comments:

Post a Comment