//Skip to content
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamefanya uchaguzi wa
wanafunzi kwenye mafunzo ya Ualimu kwa kozi za Stashahada ya Kawaida ya
Elimu ya Msingi na Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Sekondari Sayansi
na Hisabati ambayo yataendeshwa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma.
Uchaguzi huu ni kwa wale wahitimu wa
kidato cha nne kwa mwaka 2014 waliofaulu kwa daraja la Krediti na zaidi
lakini hawakupangiwa kidato cha tano.
Utaratibu wa kuripoti utatolewa na chuo husika punde watakapomaliza maandalizi ya kupokea wanafunzi hawa.
Majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 yameambatinishwa hapa.
0 comments:
Post a Comment