Friday 11 December 2015

TANGAZO KWA UMMA - UENDESHAJI WA KOZI YA STASHAHADA (DIPLOMA) YA MENEJIMENTI NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORDE – TANGA

Image result for NACTE TANZANIA
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TANGAZO KWA UMMA
UENDESHAJI WA KOZI YA STASHAHADA (DIPLOMA) YA MENEJIMENTI NA UALIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA ECKERNFORDE – TANGA


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) lina utaarifu umma kuwa Stashahada (Dilploma) ya Menejimenti na Ualimu itolewayo katika Chuo kikuu cha Eckernforde - Tanga ilipata ithibati ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na kuruhusiwa kutolewa katika kampasi yake ya Tanga. Hata hivyo imefahamika baadae kuwa chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo hayo katika kampasi zisizoruhusiwa ikiwamo vituo vya shule za msingi kwenye wilaya mbalimbali nchini. Tume ya Vyuo vikuu ilishatoa katazo la maandishi kwa Eckernforde na kwenye vyombo vya habari lakini bado fomu za kujiunga na programu hiyo zimekuwa zikiendelea kugawiwa katika vituo mbalimbali nchini.


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefanya mawasiliano na Uongozi wa Ecrkeforde ambao umedai kutohusika na fomu wala vituo hivyo vinavyoendelea kutoa fomu na kudahili wanafunzi.
Kwa notisi hii, UMMA unaarifiwa yafuatayo:
  • Kuripoti katika vyombo vya sheria uwapo wa vituo na utoaji wa fomu hizo popote unapoendelea;
  • Vituo vivyonaendesha mafunzo hayo bila kibali cha kuendesha mafunzo (ithibati) vinatakiwa kufungwa mara moja; na
  • Baraza (NACTE) na Tume (TCU) hazita watambua wahitimu wa program hiyo isipokuwa wale watakaopata mafunzo kutoka kampasi ya Tanga iliyopewa ithibati;


Ifahamike kuwa waendeshaji na wasimamizi wote wa vituo watakaopuuza agizo hili watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.


Imetolewa na kusainiwa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimuya Ufundi (NACTE)
23 Novemba 2015
Share:

0 comments:

Post a Comment