Sunday 11 December 2016

JKT: KUONGEZWA MUDA WA KUPOKELEWA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016




TAARIFA KWA UMMA

Jeshi   la   Kujenga   Taifa   kwa   mara   nyingine   tena, 
linawatangazia wanafunzi wote waliohitimu kidato cha
sita   mwezi   Mei   2016,   ambao   hawakuchaguliwa
kujiunga   na   mafunzo   ya   JKT   Mujibu   wa   Sheria
Operesheni   Magufuli   Awamu   ya   Kwanza   na
hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya
juu, kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa
kabla ya tarehe 13 Desemba 2016 .
Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linaukumbusha umma
kuwa   ni   kosa   la   jinai   kwa   kijana   aliyetangaziwa
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria
kushindwa kujiunga na mafunzo hayo.
Kosa hilo la jinai, ni kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la
Kujenga Taifa, Sura Namba 193 ya mwaka 1964 na
kufanyiwa mapitio mwaka 2002 kifungu cha 11 kifungu
kidogo cha (8).
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mwanafunzi
yeyote   atakayeshindwa   kuripoti   ndani   ya   muda
uliopangwa   wa   kuanza   mafunzo   ya   JKT   Mujibu   wa
Sheria   Operesheni   Magufuli   Awamu   ya   Pili   mwaka
2016.


Imetolewa na
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 07 Desemba 2016

Share:

0 comments:

Post a Comment