Sunday 11 December 2016

JKT: TANGAZO KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI 2016


TAARIFA KWA UMMA

1.    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawatangazia vijana wa Kitanzania wito wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na Vijana wa Kujitolea.

2.    Vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:-

      a.   Vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.
             Kundi hili linahusisha wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu  wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga vyuo vya elimu ya juu. Aidha, orodha kamili ya majina na makambi waliyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambayo ni www.jkt.go.tz  na Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz

      b.      Vijana wa Kujitolea
Kundi hili linahusisha Vijana wote waliosailiwa mwezi Mei na  Juni mwaka 2016 katika ngazi za wilaya na mkoa  na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.
3.   Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:
      a.  Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza (Dark blue) yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma isiyo na zipu, iwe na urefu  unaoishia magotini.                 

       b.  Raba ngumu za michezo zenye rangi ya kijani au nyeusi.

       c.  Shuka jozi mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari ukubwa wa 4x6.
       d.  Soksi za michezo jozi mbili rangi nyeusi.

       e.  Chandarua moja ya duara rangi ya bluu au kijani ukubwa wa 4x6.

        f.  Nguo za michezo (truck suit) jozi moja rangi ya kijani au bluu.

        g.  Fulana (T-shirt) ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote.

        h.  Mavazi hayo yasiwe ya kubana mwili.

4.  Inasisitizwa kuwa vijana wa kujitolea wanaotakiwa kuripoti makambini ni wale tu waliopita katika usaili kwenye ngazi
za wilaya na mikoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.

5.  Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na  Kujitolea wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia
tarehe 01 mpaka 05 Desemba 2016 kwa kujitegemea nauli ya kwenda na kurudi.

 BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI  2016  

BULOMBORA JKT-KIGOMA                     

      RWAMKOMA JKT -MARA         
         MSANGE JKT-TABORA

KANEMBWA JKT-KIGOMA                
                         MTABILA-KIGOMA            
          RUVU JKT-PWANI

MAKUTUPORA JKT- DODOMA                  
         MGAMBO JKT-TANGA        

MAFINGA JKT- IRINGA                                
                                       MLALE JKT -RUVUMA


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 17 Novemba 2016
Share:

0 comments:

Post a Comment