Wednesday 4 January 2017

NECTA: USAJILI WA MTIHANI WA CSEE NA QT 2017

TANGAZO


BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2017 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba;1. Kipindi cha usajili cha watahiniwa kitaanza tarehe 1 Januari, 2017 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT na kitaishia tarehe 28 Februari, 2017. Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa kuanzia tarehe 01/03/2017 hadi tarehe 31/03/2017 watalipa Shilingi 65,000/= kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi40,000/= kwa watahiniwa wa mtihani wa Maarifa (QT) ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.

2. Mtahiniwa atakaye jisajili kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2017 ni yule ambaye anarudia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) au amefanya na kufaulu Mtihani wa Maarifa (QT) katika kipindi kisichozidi miaka mitano (5) iliyopita au mwenye sifa zinazolingana na hizo alizopata kutoka nje ya Nchi na kufanyiwa ulinganifu na Baraza la Mitihani la Tanzania.


3. Mtahiniwa atakaejisajili kufanya Mtihani wa Maarifa ni yule ambaye anatafuta sifa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne kama Mtahiniwa wa kujitegemea.


4. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada ya mtihani katika ofisi za Posta pekee.


5. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz kwani mfumo wa usajili utafungwa baada ya kipindi cha usajili kumalizika.


Imetolewa na:KATIBU MTENDAJI





Share:

0 comments:

Post a Comment