Wednesday 3 September 2014

ELIMU YA UJASIRIAMALI: USINDIKAJI WA MAZAO YA NAFAKA

SOMO LA TISA : USINDIKAJI WA MAZAO YA NAFAKA


Mahindi  yaliyo  toka  kuvunwa.





















1.   USINDIKAJI  WA   ZAO  LA  MAHINDI :

Ili kuongeza matumizi ya mazao hayo na kudumisha ubora wake ni muhimu teknolojia za
kusindika nafaka zitumike. Usindikaji pia huongeza thamani ya zao.

                            

 KUSINDIKA MAHINDI

Punje za mahindi hutumika kupika makande na husindikwa kupata unga unaotumika katika
matumizi mbalimbali. Vile vile bidhaa nyingine zinazotokana na mahindi ni mafuta na wanga.

KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA

Kuna aina mbili za unga wa mahindi, unga wa mahindi yasiyokobolewa(Dona) na unga wa
mahindi yaliyokobolewa (Sembe)

 KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA

Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Debe
• Mifuko
• Chekeche ya nafaka
Jinsi ya kusindika
• Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia.
• Osha kwa maji safi na salama
• Anika kwenye chekeche safi ili yakauke
• Saga mahindi kupata unga


• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni, makaratasi yasiyopitisha
unyevu kisha hifadhi katika sehemu safi na kavu

Kumbuka: Kusaga mahindi bila kukoboa hudumisha virutubishi vilivyomo kwenye mahindi na
kupunguza upotevu wa chakula.

UNGA WA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA

Jinsi ya kusindika
• Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia
• Koboa na saga
• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni na ya karatasi isiyopitisha
unyevu.
• Hifadhi kwenye sehemu safi na kavu

Kumbuka:Kusaga mahindi yaliyokobolewa hupunguza virutubishi na wingi wa chakula kwa kiasi
cha asilimia 17 hadi 33.
Matumizi ya unga wa mahindi
Hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile ugali, uji, togwa na vyakula vya watoto.
Pia huchanganywa na shayiri na kutengeneza vinywaji kama vile bia.





Mchele  baada  ya  kukobolewa.




2.  KUSINDIKA MPUNGA
Mpunga husindikwa kupata mchele ambao pia husindikwa kupata unga.
Kusindika mpunga kupata mchele
Vifaa
• Mashine ya kukoboa
• Madebe
• Ungo
• Chekeche
• Vifungashio

Jinsi ya kusindika
• Anika mpunga juani kwa muda wa siku moja kisha uache upoe kwa usiku mmoja ndipo
ukoboe.
• Pepeta na pembua kutoa takataka kabla ya kukoboa
• Koboa kwa kutumia mashine.

Kufungasha
Baada ya kupanga madaraja fungasha kwenye mifuko isiyopitisha unyevu na hifadhi katika
sehemu kavu na safi.

Matumizi ya mchele

Mchele hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile wali, uji, biriani, mseto, pilau, bisi,
tambi na vitafunwa. Chenga za mchele hutmika kwa kutengeneza chakula cha mifugo.


KUSINDIKA MCHELE KUPATA UNGA
Vifaa
• Mashine ya kusaga
• Vifungashio

Jinsi ya kutengeneza
• Saga mchele safi kupata unga
• Fungasha kwenye mifuko safi na kavu isiyopitisha unyevu
• Hifadhi katika sehemu safi na kavu.
Matumizi ya unga wa mchele
Hutumika kupika ugali, uji na vitafunwa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye unga wa mchele ni
kama vile vilivyoainishwa kwenye virutubishi vya mchele.


3.  KUSINDIKA MTA M A / UWELE
Punje za mtama na uwele hupikwa makande na husagwa kupata unga.
 KUSAGA MTAMA/ UWELE KUPATA UNGA:
Vifaa
• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Chekeche ya nafaka
• Kichanja
• Turubai
• Vifungashio safi

 
Jinsi ya kusaga unga

• Pepeta na kupembua mtama/ uwele ili kuondoa mavumbi na takataka nyingine. Tumia
chekeche au ungo kupepeta na kupambeua
• Osha kwa maji safi kisha anika juani kwenye kichanja au turubai
• Saga kupata unga wa mtama/uwele
• Fungasha kwenye mifuko ya nailoni/ plastiki
• Hifadhi katika sehemu safi na kavu
Matumizi ya unga wa mtama/ uwele
Hupikwa ugali, uji na togwa. Vile vile htumika katika kutengeneza vyakula vya watoto






Ngano.

4.  KUSINDIKA NGANO

Ngano husagwa ili kupata unga
Vifaa
• Vifungashio
• Mashine ya kusaga
Jinsi ya kusaga
• Nyunyuzia maji kwenye ngano
• Koboa na saga ili kupata unga
• W eka kwenye vifungashio safi na visivyopitisha maji
Matumizi
• Unga wa ngano hutengeneza vitafunwa kama vile mikate, chapati, maandazi, tambi na
keki.
• Hutumika katika mapishi mbalimbali
Share:

0 comments:

Post a Comment