Wednesday, 3 September 2014

ELIMU YA UJASIRIAMALI: KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

SOMO LA NANE : KUTENGENEZA WINE YA NANASI.

Nanasi.

 Wine  ya  nanasi  ni  rahisi  kutengeneza  kwa  sababu  mananasi  yanapatikana  kwa  wingi  sana  katika  kipindi  kirefu  cha  mwaka.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  WINE  YA  NANASI.

* Nanasi.

*  Maji.

* Sukari.

* Amira.

HATUA  YA  KWANZA  KUTENGENEZA

*  Menye  maganda  ya  mananase  na  kupata  nyama . ( Kinacho  tumika  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenyewe  na  sio  maganda  ya  mananasi  )

*  Katakata  vipande  vidogo  kisha  weka  katika  chombo  kwa  ajili  ya  kuchemsha,  nanasi  linalo  faa  katika  utengenezaji  wa  wine  ya  nanasi  ni  nanasi  lenye  uzito  wa  kg. 5.

* Chemsha  kwa  muda  wa  dakika  30  kwa  moto  wa  kawaida (  Inashauriwa  kutumia  moto  wa  mkaa  )

* Baada  ya  kupoa   anza kuchachua  kwa  kuweka  amira   vijiko  vinne (  4  )  vya  chakula ,  sukari  vijiko  viwili  vya  chai na  kisha  koroga  kwa  muda  wa  dakika  20.

*  Acha  kwa  muda  wa  dakika  5  ukiwa  una  koroga  kila  siku.


HATUA  YA     PILI.

Baada  ya  siku  tano  kukamilika, chuja  wine  yako  iweke  katika  chombo  cha  kupunguza  gesi  kwa  muda  wa  siku  21.  Baada  ya  siku  21 , wine  yako  itakuwa  tayari, unaweza  kui  hifadhi  kwa  ajili  ya  matumizi.
Share:

1 comment:

  1. Je hii inaweza kudumu kwa muda gani bila kuhalibika na kuendellea kuwa salama kwa matumizi?

    Je ni njia gani sahihi ya kuihifadhi ili owe salama kwa matumizi
    Je kuna chochote cha kuchanganya ili kuifanya isihalibike?

    ReplyDelete