SOMO LA PILI : UTENGENEZAJI WA MISHUMAA.
Mishumaa., Utengenezaji wa mishumaa huweza kusaidia kuongeza kipato cha mjasiriamali, kwani bidhaa hii huitajika sana kwa matumizi mbalimbali kama vile matumizi ya majumbani nakadhalika. |
1. Paraffin Wax
2. Utambi
3. Mould ( Umbo )
4. Stearine au mixture
5. Rangi
6. Jiko la mafuta ya taa au mkaa.
7. Sufuria.
8. Boric acid.
Paraffin Wax. |
VIDOKEZO MUHIMU :
1. Paraffin Wax :
Hii inatokana na nta na sega ya nyuki iliyo changanywa na mafuta ya taa. Ina rangi nyeupe na katika utengenezaji wa mishumaa ina ubora kuliko bee wax.
* Bee Wax : Inatokana na masega ya nyuki yaliyo changanywa na mafuta ya petroli na diesel na rangi yake ni ya njano.
2. STEARINE
Hii dawa maalumu inayo fanya mishumaa iungane ama ishikamane.
Mould ( Umbo ) . Mfano wa umbo linalo weza kutumika kutengeneza mishumaa. Hata hivyo, unaweza kutengeneza umbo lolote kwa kadri unavyo taka " shape " ya mishumaa yako iwe. |
4. RANGI : Rangi nzuri zinazo tumika katika utengenezaji mishumaa ni rangi za chakula na nyingi huwa ni za maji.
Boric acid , hii ni maalumu kwa ajili ya kuufanya utambi usiishe mapema na kuufanya uwake bila kutoa moshi. |
JINSI YA KUTENGENEZA
Andaa mould ( umbo lako ) utakalo litumia baada ya kuyeyusha ( paraffin wax ) na kuchanganya na michanganyo yote.
Kwa Mfano : ( Kipimo cha stearine )
1. Wax kilo moja - Stearine vijiko vinne vya chakula.
2. Wax nusu kilo - Stearine vijiko vinne vya chakula
3. Wax robo kilo - Stearine kijiko cha chakula.
Source: Rafiki Elimu Foundation
0 comments:
Post a Comment