Wednesday 3 September 2014

ELIMU YA UJASIRIAMALI: UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE

SOMO LA TATU : UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE.

Mahindi   ni  miongoni  mwa  mazao ya  chakula  ambayo  unga  wake  unatumika  kutengeneza    unga  lishe.
UNGA  LISHE  :  Ni  unga  bora  na  unao  hitajika  sana  katika  kuborehs  afya  za  watoto, wazee  na  wagonjwa.  Ukiwa  kama  mjasiriamali  mdogo, ni  muhimu  kujua  namna  ya  kutengeneza  unga  lishe, kwani  malighafi  zinazo  tumika  katika  utayarishaji  wa  unga  huu  zinapatikana  kwa  wingi  na  kwa  bei  nafuu, hivyo  basi  hata  kwa  wewe  mwenye  mtaji  mdogo,  unaweza   kufanya  biashara  hii   bila  ya  kuhitajika  kuwa  na  mtaji  mkubwa  jambo  linalo  chukuliwa  kama  changamoto  kwa  wajasiriamali
wengi  nchini.


MCHELE.

MALIGHAFI  ZINAZO  HITAJIKA  KATIKA  UTENGENEZAJI  WA  UNGA  LISHE.

* Karanga    - Nusu  Kilo.
* Soya         - Nusu  Kilo.
* Ulezi         -   Kilo  moja  na  Nusu.
* Mahindi    -Nusu  Kilo
*Mtama     - Mtama  Nusu  Kilo.
* Uwele     -  Nusu  kilo.
* Mchele    -  Nusu  kilo..

JINSI  YA  KUTENGENEZA  UNGA  LISHE.

1. Safisha  ulezi  na  kuutoa michanga  pamoja  na  vumbi.
2. Kaanga  soya  kwenye  moto  mpaka  ibadilike rangi  na  kuwa  " brown "  ama  kahawia.
3. Kaanga  karanga  zako  na  toa  maganda.

Saga  mchanganyiko  wa   malighafi  zote  hapo  juu  kwa  pamoja,  kisha  anika  juani  mpaka  ukauke, halafu  weka  kwenye  vifungashio  kwa  ajili  ya  kuuza.

Source: Rafiki Elimu Foundation
Share:

0 comments:

Post a Comment