Tuesday, 18 November 2014

Makala: Jinsi Ya Kupata Dhamana Ya Polisi Tanzania

Kataa Uhalifuu
Dhamana inatolewa bure, hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Jambo la msingi ni mtuhumiwa kuomba apewe dhamana na kutimiza taratibu kwa muijibu wa sheria.
Vigezo vya kuzingatia kabla ya mtuhumiwa kabla ya kupewa dhamana ya Polisi
  • Polisi kujiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa, ikiwa kufika siku na saa atakayoamriwa.
  • Kujua makazi,ndugu na jamaa, ajira na ikibidi hali ya maisha ya mtuhumiwa na familia yake, kumbukumbu za kihalifu kama zipo.
  • Umuhimu wa mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana, ili aweze kujiandaa kukabiliana na tuhuma zinazomkabili kabla ya hajafikishwa mahakamani mfano kupata msaada wa kisheria
KUKATALIWA DHAMANA YA POLISI
Kifungo cha 67 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kinaeleza kwamba, mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wa Polisi anaweza kukataliwa maombi yake ya kutaka apewe dhamana
KUFUTWA KWA DHAMANA YA POLISI
Baada ya mtuhumiwa kupewa dhamana ya Polisi na kuwa huru dhamana hiyo inaweza kufutwa na mkuu wa kituo , chini ya kifungu cha 68 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai. Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha uamuzi wakufuta dhamana ni:-
(a) Kubainika kwamba mtuhumiwa anapanga mipango ya kutoroka
(b) Kwa makusudi anakiuka au yu karibu kukiuka masharti ya dhamana
ADHABU KWA KUKIUKA MASHARTI YA DHAMANA
Dhamana inayotolewa na Polisi kwa mtuhumiwa anayekabiliwa na kosa la jinai inapaswa kuheshimiwa. Kifungu cha 69 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kinatoa adhabu kali kwa mtuhumiwa na mdhamini au wadhamini wanapokiuka masharti ya dhamana waliopewa.
Share:

0 comments:

Post a Comment