Wajibu Wa Wananchi Katika Kuzuia Uhalifu
- Ukiona uhalifu unatendeka toa taarifa mapema katika kituo cha Polisi au polisi aliye karibu nawe.
- Endapo utamtilia shaka mtu au watu usiowajua toa taarifa mapema katika vituo vya Polisi,polisi wasaidizi(auxiliary police),walinzi wa amani au ofisi ya serikali ya mtaa/kijiji
- Usalama wa vyombo vya usafiri kwenye maegesho, kumbuka kufunga pikipiki au baiskeri kwa mnyororo, kuweka alamu katika magari,kuondoa vitu vya thamani ndani ya gari
- Kuwa na zizi imara la mifugo ili kuzuia wezi na kuiweka mifugo alama
- Kuepuka kusafiri na kiwango kikubwa cha fedha na vitu vyenye thamani
- Kujenga tabia ya kuweka alama kwenye vitu
- Kutoacha vitu vya thamani katika sehemu za wazi. Hata kama ni ndani ya nyumba vitu vya thamani vifungiwe ndani ya kabati au stoo.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI
- Kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani mfano kudhibiti mwendo kasi, n.k
- Kuthibitisha wanaostahili kupewa leseni za udereva
- Ukaguzi wa magari na madereva
- Kuongoza magari barabarani yaende kwa mtiririko unaostahili
0 comments:
Post a Comment