BARAZA LA MITIHANI LA
TANZANIA
TAARIFA
YA MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) MWAKA 2014
1.0 UTANGULIZI
Katika
Mkutano wake wa 102 uliofanyika
tarehe 04/11/2014, Baraza la
Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa kwa matokeo ya Mtihani wa
Kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Septemba, 2014. Watahiniwa walifanya mtihani huo kwa kutumia Karatasi
Maalum za “Optical Mark Reader- OMR”
ambazo zilisahihishwa kwa kutumia Mfumo wa kompyuta. Matumizi ya teknolojia ya OMR kwenye Mtihani
wa Kumaliza Elimu ya Msingi yalianza mwaka 2012.
2.0 USAJILI WA WATAHINIWA
Jumla
watahiniwa 808,085 wa Shule za Msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo
wakiwemo wasichana 429,624 sawa na
asilimia 53.17
na wavulana 378,461 sawa na asilimia
46.83. Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 691 walikuwa ni wenye uono hafifu,
watahiniwa 87 walikuwa ni wasioona,
watahiniwa 374 wenye matatizo ya
kusikia, watahiniwa 252 wenye
mtindio wa ubongo na watahiniwa 27
wenye ulemavu zaidi ya mmoja.
Watahiniwa
792,122 sawa na asilimia 98.02 ya waliosajiliwa walifanya
mtihani. Kati yao wasichana walikuwa 422,625 sawa na asilimia 98.37 na wavulana walikuwa 369,497 sawa na asilimia 97.63.
Watahiniwa 15,963 sawa na
asilimia 1.98 hawakufanya mtihani kutokana na sababu
mbalimbali, zikiwemo utoro na ugonjwa.
Kati yao wasichana ni 6,999
sawa na asilimia 1.63 na wavulana ni
8,964 sawa na asilimia 2.37.
3.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA
MSINGI 2014
3.1 Ufaulu kwa ujumla
Jumla
ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 waliofanya mtihani huo wamepata alama 100
au zaidi katika alama 250.
Idadi hii ni sawa na asilimia 56.99 . Kati yao wasichana ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana ni 224,909 sawa na
asilimia 60.87. Miongoni mwa watahiniwa
waliofaulu wamo wenye ulemavu 795
(wasichana 355 ambao ni sawa na asilimia 44.65 na wavulana 440 ambao ni sawa na asilimia 55.35 ya
watahiniwa wote wenye ulemavu waliofanya mtihani). Mwaka 2013 asilimia ya
watahiniwa walipata alama 100 au
zaidi ilikuwa 50.61, hivyo kuna ongezeko la
ufaulu kwa asilimia 6.38.
Mchanganuo
wa ufaulu katika madaraja mbalimbali umeainishwa katika jedwali lifuatalo:
Daraja
|
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
|
|||
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
|
Idadi
|
Asilimia
|
|
A
|
6,378
|
1.73
|
3,953
|
0.94
|
10,331
|
1.30
|
B
|
55,460
|
15.01
|
43,329
|
10.25
|
98,789
|
12.47
|
C
|
163,071
|
44.13
|
179,201
|
42.40
|
342,272
|
43.21
|
A-C
|
224,909
|
60.87
|
226,483
|
53.59
|
451,392
|
56.99
|
D
|
135,242
|
36.60
|
186,697
|
44.18
|
321,939
|
40.64
|
E
|
9,346
|
2.53
|
9,441
|
2.23
|
18,787
|
2.37
|
3.2 Ufaulu Kimasomo
Takwimu
za matokeo zinaonesha kuwa ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati
ya 0.64 na 8.94 ikilinganishwa na mwaka 2013. Watahiniwa wamefaulu zaidi
katika somo la Kiswahili ambapo
ufaulu ni asilimia 69.70 na somo
walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Hisabati
lenye ufaulu wa asilimia 37.56. Mchanganuo zaidi katika ufaulu wa masomo umeainishwa katika
jedwali lifuatalo:
SUBJECT NAME
|
YEAR
|
CLEAN
|
PASSED (A-C)
|
GRADE D
|
GRADE E
|
|||
KISWAHILI
|
2013
|
844,704
|
583,348
|
69.06
|
207,635
|
24.58
|
53,721
|
6.36
|
2014
|
791,924
|
552,003
|
69.70
|
198,993
|
25.13
|
40,928
|
5.17
|
|
KIINGEREZA
|
2013
|
844,678
|
300,001
|
35.52
|
437,695
|
51.82
|
106,982
|
12.67
|
2014
|
791,910
|
307,613
|
38.84
|
431,163
|
54.45
|
53,134
|
6.71
|
|
MAARIFA
YA JAMII
|
2013
|
844,708
|
447,657
|
53.00
|
347,014
|
41.08
|
50,037
|
5.92
|
2014
|
791,938
|
454,043
|
57.33
|
296,592
|
37.45
|
41,303
|
5.22
|
|
HISABATI
|
2013
|
844,690
|
241,741
|
28.62
|
452,937
|
53.62
|
150,012
|
17.76
|
2014
|
791,869
|
297,411
|
37.56
|
387,489
|
48.93
|
106,969
|
13.51
|
|
SAYANSI
|
2013
|
844,570
|
401,059
|
47.49
|
378,834
|
44.86
|
64,677
|
7.66
|
2014
|
791,932
|
434,679
|
54.89
|
297,167
|
37.52
|
60,086
|
7.59
|
4.0 SHULE KUMI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI
Shule 10
bora Kitaifa katika PSLE
2014 zimeainishwa katika jedwali
lifuatalo
NAMBA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI
|
MKOA
|
NAFASI
|
PS0904095
|
TWIBHOKI
|
33
|
MARA
|
1
|
PS1303065
|
MUGINI
|
40
|
MWANZA
|
2
|
PS1307121
|
PEACELAND
|
17
|
MWANZA
|
3
|
PS1304001
|
ALLIANCE
|
25
|
MWANZA
|
4
|
PS1701035
|
KWEMA
|
50
|
SHINYANGA
|
5
|
PS0501188
|
ST SEVERINE
|
53
|
KAGERA
|
6
|
PS1701064
|
ROCKEN HILL
|
58
|
SHINYANGA
|
7
|
PS0202083
|
TUSIIME
|
168
|
DAR ES SALAAM
|
8
|
PS0702252
|
IMANI
|
29
|
KILIMANJARO
|
9
|
PS1701062
|
PALIKAS
|
19
|
SHINYANGA
|
10
|
5.0 WATAHINIWA WALIOPATA ALAMA ZA JUU KATIKA MASOMO
Wapo watahiniwa walioweza kufaulu kwa kupata alama 50/50 katika
baadhi ya masomo ambapo English Language walikuwa 7,600, Kiswahili 32 na Hisabati 34. Ingawa
somo la Hisabati lina ufaulu wa
chini zaidi kuliko masomo yote, watahiniwa 34
wamepata alama 50/50 katika somo hilo ambapo kati yao Wasichana ni 08 na Wavualana ni 26 kama ilivyo
katika majedwali yafuatayo:
Orodha
ya Wasichana waliopata alama 50/50
katika somo la Hisabati.
S/No
|
NAMBA YA MTAIHINIWA
|
JINA LA MTAHINIWA
|
JINA LA SHULE
|
MKOA
|
1.
|
PS0203012-166
|
RACHEL IBRAHIMU KIUNSI
|
KIMARA-'B'
|
DAR ES SALAAM
|
2.
|
PS0203077-020
|
MARIAM WILSON CHACHA
|
PARADIGMS
|
DAR ES SALAAM
|
3.
|
PS0401041-023
|
DIANA PETER NJAU
|
ST. CHARLES
|
IRINGA
|
4.
|
PS0501188-049
|
SOFIA GIDION NGERAGEZA
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
5.
|
PS0904095-021
|
ANNABHOKE WAMBURA MAGORI
|
TWIBHOKI
|
MARA
|
6.
|
PS0904095-022
|
ATUGONZA NEWTON KAMZOLA
|
TWIBHOKI
|
MARA
|
7.
|
PS0904095-023
|
CATHERINE MOKORO MAGORI
|
TWIBHOKI
|
MARA
|
8.
|
PS1701035-041
|
EDINA NGASSA SHABU
|
KWEMA
|
SHINYANGA
|
Orodha
ya Wavulana waliopata alama 50/50
katika somo la Hisabati
S/No
|
NAMBA YA MTAHINIWA
|
JINA LA MTAHINIWA
|
JINA LA SHULE
|
MKOA
|
1.
|
PS0202109-010
|
OMEGA AMOS LUGATA
|
SABISA
|
DAR ES SALAAM
|
2.
|
PS0203058-021
|
JOHN REGINALD BUGERAHA
|
MOUNTEVEREST
|
DAR ES SALAAM
|
3.
|
PS0401043-026
|
MANSOOR MOHAMED MALAMBO
|
ST. DOMINICSAVIO
|
IRINGA
|
4.
|
PS0501188-007
|
ELIAH DANIEL MAKAMBA
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
5.
|
PS0501188-013
|
GUSTAVIUS MWOMBEKI BAGAYA
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
6.
|
PS0501188-017
|
MACHUMU NELSON SAMSON
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
7.
|
PS0501188-018
|
MAPATO MAARIFA MAGESA
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
8.
|
PS0501188-022
|
OBED LUCAS SAMWEL
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
9.
|
PS0501188-023
|
OCTAVIUS IJUMBA MTAYOBA
|
ST. SEVERINE
|
KAGERA
|
10.
|
PS0504092-004
|
DASTAN ADRIAN PIUS
|
OMUKALIRO
|
KAGERA
|
11.
|
PS0504092-009
|
DICKSON NOVATH NDAULA
|
OMUKALIRO
|
KAGERA
|
12.
|
PS0504092-015
|
MALICK AHMAD KUDABA
|
OMUKALIRO
|
KAGERA
|
13.
|
PS0504092-016
|
MATHIAS GODFREY LUGALABAMU
|
OMUKALIRO
|
KAGERA
|
14.
|
PS0504092-017
|
MICHAEL JONAS MICHAEL
|
OMUKALIRO
|
KAGERA
|
15.
|
PS0504113-021
|
ROBERT INNOCENT NOEL
|
TEGEMEO
|
KAGERA
|
16.
|
PS0702202-029
|
JUNIOR JOHNSON LOSARU
|
SCOLASTICA
|
KILIMANJARO
|
17.
|
PS0702202-042
|
SAMSON HEAVENLIGHT NKYA
|
SCOLASTICA
|
KILIMANJARO
|
18.
|
PS0904095-007
|
JAMES JOEL NYAROBI
|
TWIBHOKI
|
MARA
|
19.
|
PS0904095-017
|
ROLLY GEDI MABURA
|
TWIBHOKI
|
MARA
|
20.
|
PS0908004-020
|
EMMANUEL BENARD SARUNGI
|
BUHEMBA
|
MARA
|
21.
|
PS1101170-004
|
HAJI ADAM NJALAMOTO
|
ST. MARY'S
|
MOROGORO
|
22.
|
PS1104004-004
|
ABDULKARIM MIRAJI SAIDI
|
UHURU
|
MOROGORO
|
23.
|
PS1701035-017
|
KISHIMBA MASUNGA SHIMBA
|
KWEMA
|
SHINYANGA
|
24.
|
PS1703005-032
|
JACKSON PHANUEL MANGAIDA
|
BUGARAMA
|
SHINYANGA
|
25.
|
PS2401020-013
|
MASANJA HEZIRON KABASA
|
IHULIKE
|
GEITA
|
26.
|
PS2405080-028
|
NTOBI PAULO SUMBUKA
|
KASANDALALA
|
GEITA
|
6.0 MPANGILIO WA MIKOA NA WILAYA KIUFAULU
(a) Mikoa Kumi iliyoongoza Kitaifa ni
MKOA
|
IDADI
|
WALIOFAULU
(A-C)
|
ASILIMIA
|
NAFASI
|
DAR ES SALAAM
|
59,576
|
46,434
|
77.94
|
1
|
KILIMANJARO
|
37,918
|
26,192
|
69.08
|
2
|
MWANZA
|
53,596
|
37,017
|
69.07
|
3
|
IRINGA
|
21,363
|
14,650
|
68.58
|
4
|
ARUSHA
|
34,348
|
23,250
|
67.69
|
5
|
TANGA
|
39,066
|
26,261
|
67.22
|
6
|
NJOMBE
|
17,115
|
11,389
|
66.54
|
7
|
KAGERA
|
37,306
|
24,501
|
65.68
|
8
|
GEITA
|
27,854
|
17,560
|
63.04
|
9
|
MTWARA
|
25,015
|
15,608
|
62.39
|
10
|
(b) Wilaya
Kumi zilizoongoza Kitaifa
ni
WILAYA
|
IDADI
|
WALIOFAULU (A-C)
|
ASILIMIA
|
NAFASI
|
MPANDA MJI (KATAVI)
|
1,345
|
1,207
|
89.74
|
1
|
BIHARAMULO (KAGERA)
|
2,680
|
2,389
|
89.14
|
2
|
MOSHI(M) (KILIMANJARO)
|
3,565
|
3,145
|
88.22
|
3
|
KIBAHA DC (PWANI)
|
1,532
|
1,350
|
88.12
|
4
|
ARUSHA (M) (ARUSHA)
|
9,097
|
7,919
|
87.05
|
5
|
KINONDONI(M) (DAR ES SALAAM)
|
11,110
|
9,533
|
85.81
|
6
|
KOROGWE VIJIJINI (TANGA)
|
4,868
|
4,118
|
84.59
|
7
|
ILALA(M) (DAR ES SALAAM)
|
12,091
|
10,038
|
83.02
|
8
|
IRINGA(M) (IRINGA)
|
3,250
|
2,681
|
82.49
|
9
|
MJI MAKAMBAKO (NJOMBE)
|
2,179
|
1,785
|
81.92
|
10
|
7.0 WATAHINIWA WALIOFUTIWA MATOKEO
Baraza
la Mitihani la Tanzania limefuta
matokeo yote ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE), 2014 ya mtahiniwa
01 aliyebainika kufanya udanganyifu
katika mtihani huo. Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na watahiniwa 13 waliofutiwa matokeo yao mwaka 2013
kwa sababu za udanganyifu.
Baraza
linachukua fursa hii kuzipongeza sana Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa, Wilaya
na walimu wote waliosimamia mitihani hii kwa kuzingatia ipasavyo Kanuni za
Usimamizi wa Mitihani ya Taifa. Aidha, Baraza linawapongeza kwa dhati
watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 kwa kutojihusisha
na udanganyifu katika mitihani.
8.0 HITIMISHO
Matokeo ya Mtihani wa
Kumaliza Elimu ya Msingi, 2014 yamewekwa kwenye tovuti za Baraza la Mitihani, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ili kila mtahiniwa aweze kuona matokeo
yake. Tovuti hizo ni,
Baraza la Mitihani la Tanzania litawasilisha
Matokeo hayo kwenye Mamlaka zinazohusika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa
kujiunga na elimu ya Sekondari. Hivyo,
matokeo ya uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga na Kidato cha Kwanza yatatangazwa na Mamlaka
husika mara baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika.
Dkt. Charles E. Msonde
KATIBU MTENDAJI
0 comments:
Post a Comment