BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Wadau na Umma kwa ujumla kuwa zoezi la kupokea maombi ya kujiunga na masomo kwa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2016/2017 litafungwa rasmi tarehe 21 Novemba 2016.
Waombaji wote waliochaguliwa wanaweza kuona vyuo na programu walizochaguliwa kupitia kurasa zao binafsi au kwa kubonyeza hapa. Waombaji wote waliopangiwa vyuo wanatakiwa wawe wamesharipoti kwenye vyuo husika kwa usajili na taratibu nyingine kabla ya muda wa usajili kuisha.
Baraza linapenda kutoa nafasi nyingine kwa waliochaguliwa na wanaotaka kuhama kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kuwa wanaweza kufanya hivyo kupitia kwenye kurasa zao binafsi (profiles) kabla ya tarehe 21 Novemba 2016. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off).
Aidha, kutokana na sababu maalum maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika kozi za Astashahada (Kwa wahitimu wa Kidato cha Nne tu) na Stashahada (Kwa wahitimu wa Kidato cha Sita tu) yataendelea hadi tarehe 27 Novemba 2016. Vyuo vinavyohusika kwenye maombi haya ni Vyuo vya Ualimu vya Serikali (Government Teachers’ Colleges). Kupata sifa, nafasi na vyuo vinavyotoa mafunzo haya bonyeza hapa.
Kupata orodha ya Vyuo na programu zenye nafasi bonyeza hapa.
Imetolewana
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 19 Novemba, 2016
0 comments:
Post a Comment